0

 Mtanzania  aliyepata tuzo  ya juu duniani kwa utunzaji wa mazingira  Bw. Edward Loure amesema kazi ya kuzitetea  na kuziwezesha jamii za wafugaji zilizoko pembezoni  kupata  haki ya kumiliki ardhi inaweza kuwa nyepesi kama  wanaharakati na taasisi za kiraia zitashirikiana badala ya kushindana.
Akizungumza baada ya kuwasili nchini  akitokea  marekani  alikokwenda kupokea  tuzo hiyo akiwa mtanzania wa kwanza na mwafrika wa 27  kupata heshima hiyo  Bw. Edward Loure ambaye pia anatoka jamii ya wafugaji  amesema  ushirikiano ukiwepo  hakuna kisichowezekana. 
 
Baadhi ya wadau wanaosaidia jamii za wafugaji  wamesema tuzo aliyopata Bw.Edward  iliyoanzishwa na mwanamazingira wa kimataifa Gold Man  1989  inaonyesha umuhimu na mchango wa taasisi za kiraia katika jamii.
 
Bw.Edward Loure ambaye ni Mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Ujamaa Resource Team inayosaidia wafugaji na waokota matunda amepewa tuzo hiyo baada ya kuziwezesha jamii hizo kupata  hati za kimila  katika eneo lenye  ukubwa wa hekta  laki tano  katika mikoa ya Arusha ,Manyara, na Singida.

Post a Comment

 
Top