
DODOMA
MBUNGE wa Liwale Zubeir Kuchauka ameishangaa serikali ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kujenga kituo cha polisi wilayani
humo licha ya kuwa ina umri wa miaka 40.
Kuchauka alihoji swali hilo Bungeni jana wakati akichangia
mada kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo alisema
Wilaya hiyo ina kituo kimoja cha Polisi pia ni kibovu na kinafunikwa na
maturubai wakati wa mvua kutokana na uchakavu wake.
Alisema waziri anatoa majibu mepesi yasiyoridhisha bila
kuzingatia umuhimu uliopo katika kujenga kituo cha polisi kitakacholinda
amani.
Alisema Waziri anazungumzia ujenzi katika vituo vingine 65
ambapo yeye mbunge afikirii kama katika wilaya hizo zitakua na umri
mkubwa kama Liwale.
"Aliposema ni zaidi ya Wilaya 65 sidhani kama ina umri wa
miaka 40 kama ilivyo Liwale ina jumla km 66.000 tarafa anazosema zipo
zaidi km 60.kutoka Liwale mjini lakini hakuna kituo,"
"Hiko kituo ilichokuwepo mafaili yanafunikwa na turubai
jengo linavuja na wamepanga kwenye nyumba ya mtu binafsi ya iliyokuwa
benki ya NBC sasa nahitaji nipewe majibu ni lini kituo kitajengwa.,"
aliongeza Kuchauka
Alisema hadi sasa kuna tarafa ambazo zimekua kibiashara
zinahitaji kujengwa vituo kwa ajili ya ulinzi huku akivitaja kuwa ni
pamoja Na Kibutuka,Lilombe,Miruwi,Makata na Mkutato kuna biashara ufuta
na madini.
Awali Waziri Charles Kitwanga alisema hali ya uchumi ikiruhusu atafikiria kuwajengea kituo Liwale.
Post a Comment