MBUNGE wa Liwale Zubeir Kuchauka ameiomba Serikali kuhakikisha Wilaya
ya Liwale inanufaika na madini yanayogunduliwa katika vijiji mbalimbali
wilayani humo.
Pia amemtaka Waziri wa Nishati na Madini kutoa ufafanuzi kuhusiana na sera ya madini ili wananchi waweze kunufaika nayo yanayogunduliwa katika ardhi yao.
Alisema Liwale katika machimbo ya Kitowelo
yamegundulika madini ya Dhahabu na Safaya lakini ili wachimbaji wadogo wapate kibali cha uchimbaji ni lazima wasafiri hadi Tunduru kupata kibali jambo ambalo ni usumbufu na gharama kwao.
"Halmashauri zote hazina habari na hazinufaiki na madini hayo na wala wanaling'ombe hawajui hawapati hata sumni,huku ofisi imepelekwa Nachingwea na mapato yote ya madini yanaishia huko na Tunduru,"
"Nilitembelea mgodi huo ambao pia unamilikiwa mmiliki mmoja aliyekuwa inspekta wa Polisi IGP Omary Mahita hivyo wachimbaji wadogo wakipata madini wanampigia simu mahita anakuja kufuata na kuyapeleka kwa mauzo Tunduru ," aliongeza Kuchauka.
Kutokana na suala hilo alimuomba waziri kusimamia kuhakikisha haki ya wamaliwale inapatikana huku aliongeza kuwa hana Shaka na utendaji wa waziri na uzoefu wake lakini anashaka na utekelezaji wa bajeti hiyo.
Aliongeza kuwa Sera ya madini bado haijakaa sawa hasa pale ambapo ardhi ya kijiji imekuja kugundulika kuna madini.
Wananchi hawafahamu licha ya kua mnufaika wa kwanza anatakiwa awe yule ardhi iliyomzinguka Liwale imekua kinyume chake.
Uhaba Umeme
Kuchauka pia alizungumzia hali ya umeme na kusema kuwa tangu mwaka 1977 wilaya Liwale ulipata Umeme wa kutumia mafuta unaowashwa asubuhi na mwisho Saa nne usiku.
Alisema hayo ni mateso kwa maana kwa jiografia ya Liwale barabara mbovu hivyo hata upatikanaji wake wa mafuta ni wa tabu hasa kipindi cha mvua.
Kutokana na hali hiyo wameomba serikali iwasaidie kupata Umeme wa uhakika ili nao waweze kuutumia hata kujikwamua nao na uchumi.
Alisema bunge lisione wabunge wa kusini wanalalamika sana bungeni lakini ni kutokana na historia iliyopo ya kuonewa.
Alitolea mfano wakati wa kipindi cha mkoloni Reli ya tanga dar es salaam iling'olewa Kusini na ndio sababu ya wao kuanza kua maskini hadi wakati wa sasa.
Alisema walikua wakilima Pamba Katani Mkonge Ufuta na Korosho kwa wingi lakini baada ya reli hizo kutolewa hakuna kitu kilichoendelea hasa katika kuleta maendeleo kiuchumi.
Alisema hiyo pia ndio imesababisha kuwa na hofu hata pale ambapo imegundulia nishati ya gesi Kusini wananchi wamekosa na imani na serikali ya Chama vha Mapinduzi CCM.
"Sisi tunatabaki nyuma hadi lini ?hata nikitoa shilingi hakuna maana yeyote lkn ingekuwa inamana ningetoa shilingi wenye wizara zote kwa maana hatufaidiki nazo,"
Post a Comment