Baada ya jana Yanga kukabidhiwa kombe la VPL, leo mnyama Simba alikuwa
mjini Morogoro kutafuta angalau pointi za kumsaidia kumaliza katika
nafasi ya pili.
Katika pambano hilo dhidi ya Mtimbwa Sugar lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Simba imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wakata miwa wa Manungu, Turiani.
Bao pekee la Simba limefungwa kwa kichwa na Abdi Banda dakika ya 70 kipindi cha pili akiunganisha kwa kichwa krosi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Ushindi wa Simba dhidi ya Mtibwa ulikuwa ni ushindi wa kwanza tangu mwezi wa March. Mara ya mwisho Simba kupata ushindi kwenye ligi ilikuwa ni March 19 ilipoifunga Coastal Union kwa magoli 2-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Simba imefikisha pointi 62 ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC ambayo ipo nafasi ya pili kwa pointi 63. Miamba hiyo miwili bado inachuana kuhakikisha mmoja wao anamaliza katika nafasi ya pili, mechi zao za mwisho ndiyo zinasubiriwa kuamua nani atachukua nafasi hiyo.

Post a Comment