Baraza la madiwani kupitia wajumbe wa kamati ya fedha katika halmashauri
ya wilaya ya Gairo wamesusia kikao cha kupitisha bajeti kilicho
andaliwa na mkurugenzi wa wilaya hiyo kufuatia baraza la madiwani wa
halmashauri hiyo kuazimia kutokuwa na imani na mkurugenzi
Wakiongea na channel ten baada ya kikao hicho kuvunjika, wajumbe hao wa kamati ya fedha wameeleza kushangazwa na hatua ya mkurugenzi huyo kuwaitisha kikao maalum cha kujadili na kupitisha bajeti bila kujadili na kupitia miradi ya maendeleo na kwamba hawatakuwa tayari kufanya kazi na mkurugenzi huyo kwa namna yoyote ile hadi hapo maazimio yaliyofikiwa na kikao cha mei 07 mwaka huu na wajumbe wa baraza la madiwani yatakapo fanyiwa kazi.
Channel ten ilifika hadi kwa mkurugenzi wa halmashauri ya gairo kibwana magota ili kujua kinagaubaga juu ya tuhuma hizo dhidi yake ambapo aligoma kuzungumza chochote kwa madai hakuwa na makubaliano ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Post a Comment