1: Madoa kutokana na Bakteria (Bacterial spot)
Dalili za madoa yatokanayo na bakteria hutokea kwenye majani, matawi na kwenye matunda ya nyanya.
DALILI.
Dalili bayana zaidi huonekana kwenye majani, ndio maana ya hilo jina
‘Madoa ya majani kutokana na bakteria’. Makovu madogo ya rangi ya
manjano-kijani hujitokeza kwenye majani machanga na matokeo yake ni
majani yaliyopindapinda, yaliyokoza, yaliyotota na yenye kuonesha ishara
kama yenye mafuta kwenye majani yaliyokomaa.Makovu hukua haraka na yanaweza kufikia ukubwa wa 0.25-0.5 sm, huwa na rangi ya kahawia/nyekundu. Umbo la makovu kwa kawaida huwa na pembe kwa vile hufuata umbile la mishipa midogo ya majani. Makovu mara nyingi hutokea kwenye ncha na pembezoni mwa jani ambamo unyevu huhifadhiwa.
Katika hali ya ujoto/ukavu, majani huonekana yamechanika chanika kutokana na maeneo ya pembezoni mwa majani na kati ya makovu hukauka na kukatika. Ukubwa wa makovu huongezeka kutokana na muda ambao majani yanakuwa na maji. Kwenye matunda, madoa huanza kwa kuwa na rangi ya kijani kibichi na kuonyesha sehemu kama.
zilizotota maji. Kwa kawaida hufikia ukubwa wa 0.5 sm. Madoa haya hatimaye huwa yenye mnyanyuko, rangi ya kahawia na yenye kukwaruza kwenye tunda la nyanya. Madoa haya kawaida hufanya njia za kupenya aina nyengine za ukungu na bakteria wavamizi na kusababisha kuoza kwa matunda.
UDHIBITI
Madoa ya majani yanayosababishwa na bakteria yakishaingia tu shambani au kwenye jengo la kuoteshea mimea ni vigumu kuyadhibiti. Mbinu zifuatazo zinaweza kuchukuliwa kudhibiti ugonjwa huu:
Mbinu bora za kilimo
- Mbegu zisizo na vimelea vya magonjwa.
- Miche isiyo na magonjwa .
- Mzunguko wa mazao.
- Epuka maeneo yaliyopandwa nyanya kwa muda wa mwaka mmoja.
- Tumia miche iliyopasishwa.
- Ondosha shambani na choma moto mabaki ya mimea iliyoathirika na masalio.
- Safisha na kuua vimelea vya magonjwa katika vitalu kabla ya kusia mbegu.
Kibaiolojia: Virusi vinavyoshambulia bakteria hudhibiti magonjwa haya, lakini ni lazima viwekwe shambani wakati wa jioni angalau mara mbili kwa wiki. Bakteria wa jamii ya Xanthomonas ambao hawasababishi magonjwa hutoa udhibiti wa kiasi wa madoa yanayosababishwa na bakteria.
2: Mnyauko kutokana na bakteria (Bacterial wilt)
Dalili za awali ni kunyauka kwa majani ya kwenye ncha. Baada ya siku mbili dalili hii huwa ni ya kudumu, na mti wote hunyauka na kufa kutokana na kuendelea kwa ugonjwa. Matawi yote hunyauka kwa wakati mmoja. Shina la mti ulionyauka likikatwa shehemu ya kati huwa na rangi nyeusi na huonekana kama iliyotota maji. Shina linapokamuliwa, hutoa maji ya utelezi kijivujivu unaotiririka.
Hatua zinazofuata za ugonjwa huu ni kuoza kwa sehemu ya kati ya shina na hii husababisha uwazi katika sehemu hiyo. Mzizi ulioathirika huoza na kuwa na rangi ya kahawia mpaka nyeusi. Mnyauko wa bakteria hausasababishi madoa kwenye matunda.
Mmea hunyauka ukiwa na rangi ya kijani, (majani hayawi ya njano au kuwa na madoa) na inaweza kutokea ghafla. Katika hali ya ugonjwa kusambaa taratibu, mti hutoa mizizi mingi juu ya shina na mmea hudumaa. Kuanguka kabisa kwa mmea hutokea wakati nyuzi joto zinapofikia 320C au juu ya hapo.
UDHIBITI
Mnyauko unaosababishwa na bakteria unaweza kutambuliwa shambani kwa kukata sehemu ya chini ya shina urefu wa 2-3 sm na kuisimamisha kwenye glasi ya maji. Ikiwa ugonjwa upo, basi michirizi ya bakteria kama nyuzi hutoka kwenye kipande hicho cha shina sekunde chache tu baada ya kukisimamisha kwenye maji.
Mbinu bora za kilimo
- Mzunguko wa mazao na yale ambayo hayaathiriki.
- Usipande nyanya katika udongo ambao ugonjwa huu uliwahi kuwemo.
- Tumia aina za mbegu zenye kustahimili/zisizopata ugonjwa wa mnyauko bakteria. (Kama vile Fortune Maker, Kenton na Taiwan F1).
- Toa na angamiza mimea iliyonyauka kutoka shambani kupunguza usambaaji wa maradhi.
- Ruhusu mafuriko yenye kuenea.
- Ongezea mbolea ya samadi.
- Panda katika msimu ambao si rafiki kwa ugonjwa huu.
- Zuia minyoo fundo (root-knot nematodes) kwani husaidia uingiaji wa ugonjwa.
- Changanya na mazao jamii ya kunde.
- Epuka kutumia ardhi kwa miaka 3-4 baada ya uzalishaji wa nyanya.
Kemikali: Mnyauko wa Bacteria unaweza kudhibitiwa kwa kutumia Chlorothalonil (Bravo 720/Ensign, Bravo Ultrex, Bravo Weather Stik, Echo 720, Echo 90DF, Echo Zn, Ridomil/Bravo). Juu ya hivyo, tahadhari inapaswa ichukuliwe kuepuka usugu wa vimelea vya ugonjwa, hivyo mbinu ya matumizi ya kemikali katika kuzuia ugonjwa inabidi ichanganye na mbinu nyinginezo.
Kibaiolojia: Kuzuia kunyauka kunakosababishwa na bakteria kunajumuisha matumizi ya ardhi zenye kuzuia ugonjwa na ardhi zenye vimelea wapinzani (km. Candida ethanolica, Pythium oligandrum).
Post a Comment