Serikali katika
mkoa wa Gansu, China imeagiza wasimamizi wa shule kutekeleza kikamilifu
marufuku ya kutokubalia shughuli zozote za kidini shuleni.
Wizara
ya elimu katika mkoa huo uliopo kaskazini mashariki kwa nchi hiyo
imechukua hatua hiyo baada ya msichana mmoja kuoneshwa kwenye video
akikariri vifungu kadha vya Koran katika shule moja.
Shule hiyo imeshutumiwa vikali na maafisa hao wa wizara ya elimu.
Wizara hiyo kupitia taarifa imesema dini shuleni huathiri hali ya kiakili ya watoto.
Baadhi ya shughuli za kidini hukubaliwa nchini China lakini hudhibitiwa vikali.
Lakini
waandishi wa BBC nchini humo wanasema serikali huwa makini sana kuhusu
baadhi ya shughuli za kidini ambazo zinaweza kuathiri utambulisho wa
kitamaduni wa Kichina.
Post a Comment