Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster akiwapongeza washiriki wote
waliojaza fomu za kushiriki shindano la mama shujaa wa chakula msimu wa
tano 2016 kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Afisa
uhakiki wa ubora kutoka TBS Stela Mroso akisisitiza jambo kuhusu
ushirikiano wao kama Shirika la Viwango la TBS na Oxfam Tanzania
kuhakikisha wanatetea wanawake
Mwakilishi kutoka
Wizara ya Kilimo Paskarina Kayuma akitoa Shukurani kwa Shirika la Oxfam
Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyua wanawake katika kilimo na amewaomba
juhudi hizo ziendelee.
Miongoni mwa
majaji Fredy Njeje kutoka Blogs za Mikoa na Edna Kiogwe mshiriki wa
mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita(ambaye hayupo pichani)
wakielezea namna usaili ulivyofanyika mpaka kuwapata washiriki 19
katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano kwa mwaka 2016
Aliyekuwa mshiriki
wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita Ester Kulwa
akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Mabalozi wa
Chakula na Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam kwa
upande wa Tanzania Shamim Mwasha ambaye pia ni Fashion Blogger(wa
kwanza kushoto), Jacob Stephen 'JB' Msanii Maarufu wa Bongo Movie(wa
katikati) na Khadija Mwanamboka wakitangaza majina 19 ya washiriki wa
shindano la Mama shujaa wa chakula 2016 msimu wa tano.
Baadhi ya
wageni wakiwa katika Hafla fupi ya kutangaza majina 19 ya washiriki
katika shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016
Aliyekuwa Mshiriki
wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pili akizungumza jambo wakati wa
Hafla fupi ya kutangaza washiriki shindano la Mama shujaa wa chakula
msimu wa tano 2016.
Suhaila Thawer ambaye ni 'Public Forum Officer' kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akitoa neno la Shukurani
Meneja utetezi kutoka Oxfam Tanzania Eluka Kibona akitoa maelezo kuhusu
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa
wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa
chakula.
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa
wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa
chakula.
Mabalozi
wa Chakula na Kampeni ya Grow wakiwa katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Jane Foster (wa kwanza Kulia)
Baadhi
ya akina mama waliowahi kushiriki shindano la Mama shujaa wa Chakula
Misimu iliyopita wakiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Jane
Foster (wa pili kulia)
Hatimaye 19 watajwa kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa tano kwa mwaka huu 2016, ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima wanawake kote nchini, fomu 1795 zilipitiwa na kuwapata washiriki hao ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili kuhakiki iwapo kile walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi. Mashindano
ya Mama Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha
Enguiki kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na kurushwa katika Runinga ya ITV.
Akizungumza wakati wa kutangaza majina hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ni muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema katika uchambuzi wa fomu hizo walikuwa ni wanawake wakulima ambao wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wadogo wadogo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster alisema shindano hilo limeanza
kuendeshwa kuanzia mwaka 2011 na sasa ni msimu wa tano na limefanikiwa
kuwaunganisha wanawake wakulima wadogo wadogo ambao ni asilimia 70 ya
wanawake nchini. Alisema majaji wamefanya kazi
ya
kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi
wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe.
Alisema
majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki
ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto
zilizopo zitatuliwe. Aliongeza kuwa shindano la mama shujaa wa Chakula
linaendeshwa katika nchi tatu Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia na
Tanzania. Ambapo Tanzania wamepita katika mikoa mbalimbali na kukusanya
wanawake wakulima wadogo wadogo ambao tunaamini
kwa kuwa pamoja wanaweza kupaza sauti kwa watunga sera kuhusu changamoto wanazokutana nazo.
Afisa
Uhakiki wa Ubora TBS, Stela Mroso alisema shirika la viwango nchini
liliungana na Oxfam mwaka jana ili kuhakikisha wanawaleta wanawake
pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu kilimo chenye ubora na mazao
yanayoweza kuwa na viwango vya kimataifa.Alisema bila viwango wanawake
hawawezi kufanya biashara, huku akitoa wito kwao kujitokeza
ili kuangalia ubora wa mazao wanayozalisha. Aliongeza kuwa asilimia 80 ya
wanawake nchini wanajishughulisha na Kilimo kwa hiyo ni muhimu chakula
kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa Kimataifa.
Washiriki
wa Mama Shujaa wa Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa
Morogoro, Monica Charles Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema Gilbet Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39) Mkoa wa Singida, Anjela
Chogsasi Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa
wa Shinyanga, Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa Kaskazini Unguja,
Christina Machumu (42) Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa
wa Kagera. Mary Bony Soko (42) Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39)
Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini
Magharibi,
Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu (30) Mkoa
wa Rukwa, Mwajibu Hasani Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa Songwe, Hidaya Said Musa (40) Mkoa wa Tanga na Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.
Post a Comment