Kaimu Ligoma wa pili kutoka kushoto na Jonson Mpilimba wa pili kutoka kulia
kusho ni Yahaya Husseni na Mukisini Kinderu wa pili kutoka kulia
Mgeni rasmi Bw.Hassani Mpako akiongea na wadau wa masumbi mara baada ya kumalizika kwa pambano.
Jana wakazi wa wilayani Liwale
mkoani Lindi walishudia mipambano miwili mkali sana ya ngumi (Boxing)
iliyowakonga yoyo za washabiki wa mchezo
wa masumbi kwani kulikuwa na ugeni kutoka jijini Dar es salaam kuja kupambana
na mabondia wa Liwale.
Katika mchezo wa kwanza wa
masumbi uliofanyika jana usiku katika ukumbi wa LENAR CLUB uliwakutanisha
bondia kutoka Liwale Kaimu Ligoma Vs Jonson Mpilimba kutoka jijini dare s
salaam ambao uzito wao ulitofautiana Ligoma alimzidi Mpilimba uzito wa kila 6.
Mpambano huo ulikuwa na Round 6
mwazo wa mchezo katika roundi ya kwanza kila mchezaji aliweza kumsoma mwezake
jinsi mbinu anayotumia na kusoma makosa ya mwezeke,roundi ya 3 na ya 5 mpambano
ulikuwa mkali sana kwani kila mtu alikuwa yupo makini sana huku mashabiki
wakiwa na kiu ya kumfahamu nani atashinda juu ya pambano hilo.
Roundi ya 5 Kaimu Ligoma
aliitumia vizuri baada ya kumpunguza nguvu Jonson Mpilimba kwa mtwanga makonde
maziko na Mpilimba kupelekea kushindwa kuimili hayo makonde lakini alijikakamua
mpaka kumaliza roundi hiyo ya 5.
Katika roundi ya 6 hapa mpambano
ndio ulikuwa mkali zaidi huku bondia Kaimu Ligoma alishangiliwa na mashabiki
wengi ambao kelele zile zilimfanya
aongeze juhudi zaidi ya kushinda kwani ikizingatia wakazi wengi walienda kuona
ndugu zao watawashinda watu wa jijini Dar es salaam kitendawili hiko kiliweza
kuteguliwa namo roundi ya 6 baada ya Ligoma kumtandika Jonson Mpilimba na
majaji wa mchezo huo waliweza kutoa pointi
Jaji wa kwanza aliweza kutoa
pointi kama ifuatayo-;
1. Kaimu
ligoma alipewa pointi 51-29 Jonson
Mpilimba
2. Kaimu
ligoma alipewa pointi 51-29 Jonson
Mpilimba
3. Kaimu
ligoma alipewa pointi 51-29 Jonson
Mpilimba
Kwa matokeo haya Kaimu Ligoma
kutoka wilayani Liwale alitangazwa mshindi wa pambano hili.
Pambano la pili likafuata nalo
nilikuwa linasubiliwa kwa hamu sana baada ya kuwakutanisha mkongwe wa masumbwi
kutoka hapa wilayani Mukisini Kinderu Vs Yahaya Husseni kutoka jijini Dar es
salaam huu mchezo ulikuwa na jumla ya
round 8.
Mchezo huu ulichezwa katika round
3 tu na mshindi akatangazwa katika roundi ya kwanza na ya pili mchezo ulikuwa
mzuri sana kwani kila mmoja alionesha uwezo wake mbele ya mashabiki waliojaa
ndani ya ukumbi wa LENAR CLUB na kuweza kukonga nyoyo za mashabiki wa ngumi.
Katika roundi ya 3 bondia
Mukisini Kinderu aliweza kuonesha uwezo wake mbele ya mashabiki waliofika
uwanja hapa baada ya kupiga mpizani wake Yahaya Husseni na kupelekea bondia Yahaya kugeguta mkono na kushindwa
kuendelea na mpambano huo ndio majaji waliweza kumtangaza mshindi bondia
Mukisini Kinderu na kuwafanya wapenzi wa
masumbi hususani wakazi wa Wilayani Liwale kujawa na furaha zaidi baada ya
wachezaji wao kuweza kushinda mapambano yao yote.
Mara baada ya kumalizika kwa
mpambano washiriki wote waliongea na Mwandishi wa habari wetu kuzungumzia juu
ya mchezo huo kwa pande zote zili pamoja na waliwalimu wao nao walihojiwa.
Bondia Jonson Mpilimba alisema
amekili kushindwa kwenye mpambano wake dhidi ya mpinzani wake Kaimu Ligoma japo
alizidiwa uzito wa kila 6 lakini aliongeza kusema anajipamba upya na kama
kutakuwa na pambano lijalo ataweza kushinda nae Kaimu Ligoma alisema amesikia
furaha zaidi kuitanza Liwale kwa ushindi alioupata pia alibainisha siri ya
ushindi wake ni kushiriki mazoezi na kuzingatia maelekezo ya mwalimu na kusema
mchezo wa bondia si mchezo wa kubezwa kwania ni moja ya mchezo wa kujenga afya
ya mwili na amewaomba wadau mabalimbali kujitokeza kuweza kusaidia mchezo huo.
Mukisini Kinderu alisema huu
ushindi ni zawadi tosha kwa wakazi wa Liwale hii kwani vijapaji zipo na watu wa
wialayani wanavipaji amewaomba viongozi
na wadau kuweza kuzamini mashindano mabalimbali ili kuweza kutoa fursa na
kujenga ushirikiano nae bondia Yahaya Husseni alisema pambano hili ameshindwa
na kilichotoa ndio matokeo ya mchezo lakini hakati tamaa ataendelea kujipanga
na anatamani kukutana nae Kinderu kwa pambano jingine.
Mbwana Amdani ni kocha wa mabondi
Jonson Mpilimba na Yahaya Husseni wa kutoka jijini Dar es salaam alisema
mchezo wa jana ulikuwa mzuri japo wanafunzi wake wameshindwa mapambano yote
lakini ataweza kuboresha makosa yaliotokea kwa mwanafunzi pia aliongeza kusema kila siku akiomba
pambano na Mukisini Kinderu siku zote kideru huwa anamkimbia aliopoulizwa na
mwandishi wetu bondia Kinderu alikataa madai hayo na kusema yeye amuogopi na
yupo tayari kupambana nae.
Nae kocha wa mabondia kutoka wilayani
Liwale Amiri Kolela na mzamini wa pambano hilo alisema mchezo ulikuwa mzuri na
siri ya kushindi walisema walijiandaa kwa ndani ya miezi 3 kwani hakutaka
kufanya vibaya kwakuwa mpambano huo unafanyika nyumbani,ushindi waliopata ni
zawadi tosha kama vijana wa Liwale wanauwezo mkubwa.
Kolela alitoa wito kwa vijana
wajitokeze kushiriki katika michezo yote ili kujenga afya pia alibainisha kama
vijana watashiriki katika mchezo matumizi ya madawa ya kulevya yataisha na
vijana watakuwa na mawazo chanya ya kimaendeleo pia michezo ni kitu muhimu sana
kwani mchezo hujenga urafika katika maeneo mbalimbali ya nchini.
Kolela aliweza kubainisha
changamoto mbalimbali za mchezo huo alizitaja baadhi ya changamoto kama vile
kukosa sapoti kwani wanatamani kufanya mapambano mengi sehemu mbalimbali lakini
inashindikana baada ya kukosa sapoti hivyo amewaomba wadau wa michezo
kujitokeza kuweza kusapoti mchezo huo kwa kila mchezo unafaida na ni ajira.
Changamoto ingine ni uhaba wa
vifaa vya michezo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuweza kuwasaidi ili
waweze kufanya mazoezi zaidi lakini japo kuwa kuna uhaba wa vifaa na changamoto
hawakati tamaa wanaendelea na mazoezi.
Mgeni rasmi wa pambano hilo ni mwenyekiti wa chama cha ushirika Umoja Mh.Hasani Mpaka alisema yupo tayari
kutatua changamoto zinazowakabili wanabondio hao hivya amewaahadi kuwapatia
baadhi ya vifaa muhimu vinavyohitajika muda
huu alionfgeza kutoa ahadi atazami pambano moja kubwa ili vijana kuweza
kuonesha vipaji vyao na kuweza kuwashawishi vijana mbalimbali kupenda michezo
na kuona faida ya watu kushiriki katika michezo.
Pia amewatoa wasiwasi wanabondia
na mashabiki wote walioudhulia mchezo huo juu ya bondia Yahaya Huseni
aliyeteguka mkono atamlipia huduma zote za matibabu.
Post a Comment