Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim
Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna
mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.
Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa.
Hata hivyo, Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote gerezani hapo.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama ulinzi na usalama wao umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa anayetoweka.
Amesema matumizi ya dawa hizo yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani watumiaji wengi ni vijana,hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua wauzaji na watumiaji.

chanzo:jamiiforums
Post a Comment