TAARIFA KWA NYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam – 11 April 2016 –fastjet,
shirika la ndege la gharama nafuu barani Afrika imeshinda Tuzo ya
Shirika la Ndege Linaloongoza Afrika kwa Gharama Nafuu kwenye Tuzo
ya 23 ya Mwaka ya Usafiri Duniani iliyotolewa Zanzibar,
Tanzania Aprili 9, 2016.
Tuzo
ya Usafiri ambayo inatambulika duniani imepangwa kwa kutambua,
kutuza na kusherehekea mafanikio kwenye sekta zote muhimu za
usafirishaji wa kwenye sekta ya utalii.
Tuzo
ya Shirika la Ndege Linaloongoza kwa Gharama Nafuu ambayo hutolewa kwa
wataalamu wa usafiri na utalii pamoja an watumiaji duniani
kote inatokana na kutambua huduma za fastjet za kufanya watu wamuumudu
usafiri wa anga, usalama na kuaminika kwenye mtandao yote barani
Afrika.
“Kutambuliwa
na kupata tuzo hii sio tu kunaonesha kujituma kwa ufanisi kwenye
usafiri wa anga, lakini kunaonesha matokeo ya juhudi zetu tunazojaribu
kulifanyia bara la Afrika,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet
Tanzania, John Corse na kuongeza, “tunajivunia sana kupokea
kutambuliwa huko na sekta hii kubwa na fastjet itaendelea kuufanya
usafiri wa anga kuwa wa gharama za chini ambazo watu wengi
watazimudu barani Afrika.”
Shirika
hilo la ndege la bei nafuu lilizinduliwa Novemba 2012 na linafanya
safari kadhaa za ndani ya Tanzania kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya,
Mwanza na Kilimanjaro. Kukua kwa mtandao wa fastjet pia kunatoa
huduma kwa njia ya kutoka Dar es Salaam na Zanzibar na kwenye vituo vya
kimataifa kama vile Johannesburg, Harare, Victoria falls, Entebbe,
Nairobi na Lusaka.
Fastjet
inatarajia abiria wake wengi kwenye njia hizo inakotoa huduma kuwa
ndio wanasafiri kwa mara ya kwanza kwa kutumia ndege kutokana na sababu
ya kukwazwa na tozo za nauli ya juu ambazo awali hawakumudu kulipa
kwa ajili ya usafiri huo.
Huduma
hii ya nauli nafuu imeungwa mkono kwenye utafiti uliofanywa na shirika
hilo hivi karibuni, unaoonesha kuwa asilimia 40 ya abiria kwenye njia
zote walikuwa ndio mara yao ya kwanza kusafiri kiumudu kusafiri kwa
ndege kwa mara ya kwanza hivyo pongezi ziende kwa gharama nafuu za
fastjet.
Jambo
jingine ambalo linapatikana kwenye njia inamopita fastjet ni
kuboreshwa kwa mbadala wa mzigo ambako kunajulikana kama ‘freighty’
kunakoruhusu abiria kusafirisha hadi kilo 80 zilizofungwa kwenye
mabegi kwa gharama ya shillingi 88,000. Mbadala huo wa kusafirisha
mizigo kimsingi umekuwa ni maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na
fastjet kwenda kununua bidhaa za jumla kimataifa na kuzisafirisha kwa
ajili ya kuziuza kwenye masoko ya nyumbani mwao.
Tuzo
hii inaongeza idadi ya tuzo ambazo fastjet
imeshazipata zikiwemo kushinda Tuzo ya Ubunifu kwenye Usafiri kwenye
utoaji wa nane wa tuzo hiyo mwaka 2015, na hali kadhalika kutangazwa
kuwa shirika la ghama nafuu barani Afrika katika
kulinganishwa mengine kwenye usafiri wa anga kupitia mtandao wa
safiri WhichAirline.com in 2016.
Post a Comment