0

Watu watano wamenusulika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya kwa moto katika ajali ya gari mbili zenya shehena ya mafuta zilizoteketea kwa moto wakati wakihamisha mafuta kutoka gari iliyopata ajali katika mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda kutokana na ukosefu wa vifaa vya zima moto kwenye mipaka ya nchi wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Ajali hiyo iliyotokea jumapili majira ya saa 12 jioni baada ya gari lenye shehena ya mafuta kunusulika kuanguka kwenye mtaro na kuegama kwenye kingo za barabara ya Benako Rusumo ambapo wahusika walilazimika kuhamisha mafuta kwa Jenereta kupakia gari nyingine ili kuwezesha gari hilo lipate wepesi na kwamba wakiwa katika harakati za kuhamisha mafuta mipira ilimwaga mafuta kwenye jenereta na kusababisha mlipuko wa moto.
 
Kufuatia ajali hiyo watu watano wamejeruhiwa vibaya kati yao wanne wamefahamika kuwa ni raia wa nchi ya Rwanda na mmoja mtanzania mkazi wa Benako Ngara kama wanavyobainisha mashuhuda wa ajali hiyo.
 
Akithibitisha kupokea majeruhi wannne raia wa nchi ya Rwanda kaimu mganga mfawidhi hospitali ya wilaya ya Ngara Nyamiyaga Dkt William Munyonyela amesema kati ya majeruhi wanne mmoja anahali mbaya atapelekwa hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ngara Bi Honorata Kitanda amebainisha changamoto zilizopo katika maeneo ya mipaka ya nchi kutokana na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto

Post a Comment

 
Top