Ofisi
ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu imebaini Wizara ya Nishati na
Madini na shirika la maendeleo ya Petroli hayana mfumo wa kuzingatia
ufanisi, ubora na maadili katika kusimamia mchakato wa utoaji wa
mikataba na leseni kwa makampuni ya utafutaji mafuta na gesi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi ripoti za
ukaguzi za mwaka 2014/15 kwa Spika wa bunge. Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa
hesabu za serikali Prof.Mussa Asaad amesema wizara ya nishati na madini
haina mpango wa ufuatiliaji, tathimini na utoaji taarifa za utendaji wa
uendelezaji ikiwemo rasilimali watu katika sekta ya mafuta na gesi
asili nchni.
Kuhusu sakata la umiliki wa kampuni ya usafiri Dar es Salaam UDA
Profesa Asaad ameitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria bodi ya
wakurugenzi wa UDA kwa kuuza hisa za shirika hilo bila kupata kibali cha
serikali pamoja na kutoa punguzo la asilimia 60 kwa hisa za mwekezaji.
Aidha kuhusu deni laTaifa amesema linakuwa kwa asilimia 27 wakati
uchumi haukuwi kwa kiwango hicho na kusababisha malipo kwa ajili ya
madeni yanatumia zaidi ya asilimia 46 ya pato la taifa ukujumlisha na
malipo ya mishahara yanaweza maliza bajeti yote ya nchi.
Post a Comment