Wakimbizi watoroka kambini DRC
Kambi 5 za
wakimbizi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zimesalia mahame
baada ya wakimbizi kutoroka vita vilivyozuka katika eneo la Kivu
Kaskazini.
Umoja wa mataifa unaoendesha kambi hizo 5 unasema kuwa
mapigano yalizuka katika mji wa Mpati na kusababisha zaidi ya wakimbizi
35,000 kutoroka ilikuokoa maisha yao.UN inahofia usalama wa wakimbizi hao wa ndani kwa ndani.
Jeshi la taifa limekuwa likikabiliana na waasi waliojihami.
Post a Comment