Timu ya VIJUSO Vs BLACK STAR
Ligi ya mbuzi Vijana Cup inayofanyika wilayani Liwale mkoa wa Lindi (Liwale mjini) jana april 29 katika kundi A kulikuwa na mchezo mkali wa aina yake mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano kati ya timu NANGANDO Vs KOMBAINI.
Katika mchezo huo timu ya Kombaini iliweza kushinda goli 2 kwa Bila dhidi ya Nangando huku magoli yote yakifungwa katika kipindi cha pili cha mchezo.
Leo april 30 katika kundi B kulikuwa na mchezo kati ya VIJUSO Vs BLACK STAR mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano,katika kipindi cha kwanza timu ya Black star ilikuwa ikiongoza goli 2 kwa 1.
Katika kipindi cha pili mchezo ulikuwa wa aina yake namo dakika ya 52 Vijuso waliweza kusawazisha goli na waliweza kuongeza goli la tatu katika dakika ya 65 na ndani ya dakika ya 81 kulitokea na vurugu za wachezaji kwa wachezaji na kulazimika mchezo kusimama kwa muda wa dakiaka 5 na mwamuzi wa mchezo waliweza kutoa kadi nyekundi kwa kila mmoja aliyeanzisha vurugu na kupekea kila timu kuwa na pungufu ya mchezaji mmoja mmoja na kulazimika kucheza kila timu wakiwa 10.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinakamilika matokeo yalikuwa VIJUSO 3-2 BLACK STAR
Liwale Blog iliongea na kocha wa timu ya Black Star, Fadhili Mbugila alisema matokeo hakuridhika nayo kutokana na vurugu zilizojitokeza uwanjani hapo na alisema hali ya vurugu zilizojitokeza leo zisijitokeze tena kwa siku za mbele.
KESHO KATIKA KUNDI A KUTAKUWA NA MCHEZO KATI YA TIMU YA Z.F.C Vs LIKONGOWELE
KUNGALIA MATOKEO YOTE YA LIGI YA MBUZI VIJANA CUP >>BOFYA HAPA
Post a Comment