0
Kwa watu wangu mashabiki wa soka la Ligi Kuu Uingereza, leo April 30 2016 imechezwa michezo 6 ya Ligi hiyo, huenda hukupata nafasi ya kuona michezo hiyo, ambapo mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Norwich City ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kuchezwa April 30 2016.
Arsenal ambao walikuwa katika uwanja wao wa Emirates wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kufikisha jumla ya point 64 katika mechi zao 36 walizocheza msimu huu na kusalia nafasi ya 3 wakiongozwa na Leicester City mwenye point 76 na michezo 35.
2285
Tottenham Hotspurs wapo nafasi ya pili wakiwa na point 69 na michezo 35, goli la Arsenal lilifungwa na Danny Welbeck dakika ya 59. Arsenal sasa anakuwa amebakiza michezo miwli ili atimize jumla ya mechi zake 38 za Ligi Kuu msimu huu. Ushindi wa Arsenal haukusaidia mashabiki kuacha kubeba mabango ya kushinikiza Wenger aondoke.
<> at Old Trafford on August 26, 2013 in Manchester, England.
Matokeo ya mechi za Ligi Kuu Uingereza leo April 30 2016

Post a Comment

 
Top