0
                   
Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys April 5 2016 ilileta faraja kwa watanzania, baada ya kuendeleza umahiri wake wa kuifunga timu ya taifa ya vijana ya Misri The Pharaohs mara mbili mfululizo.

Serengeti Boys ilirudiana kwa mara ya pili na timu ya taifa ya Misri na kufanikiwa kuifunga kwa jumla ya goli 3-2, ushindi huo unakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka Serengeti Boys iwafunge Misri kwa jumla ya goli 2-1, magoli ya leo ya Serengeti Boys yalifungwa na Ibrahim Abdallah dakika ya 28, 60 na Boko Seleman aliyefunga dakika ya 36.

Wakati magoli ya Misri yalifungwa na  Ahmed Saad dakika ya 22 na Diaa Wahid aliyefunga goli la pili dakika ya 74, mchezo huo unatajwa kuwa na mvuto na timu zote ziligawana kuutawala mchezo kwani Serengeti ilitawala kipindi cha kwanza.
                                         

Post a Comment

 
Top