Furaha ya mwanzo mwema
Timu za Barcelona na Bayern Munich zimeanza vizuri michezo yao ya kwanza ya hatua ya robo fainali ya klabu bingwa ulaya.
Barcelona,
wakicheza katika uwanja wao wa Camp Nou,wamechoimoza na ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid, mshambuliaji Luis Suarez akifunga
mabao yote mawili.
Na bao la Atletico Madrid likifungwa na
Fernando Torres ambae pia alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya
kupewa kadi mbili za njano.
Nao Bayern Munich wakiwa wenyeji wa Benfica wameshinda kwa bao 1-0 kwa bao lilowekwa kambani na kiungo Arturo Vidal.
Post a Comment