Bi. Shakira Mkoyage akisoma risala ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Zahanati ya Mkoyage hapo jana april 29 mbele ya mgeni rasmi Mh. Ephraim Mmbaga,mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Zahanati hiyo kuanzia ujenzi wake na ununuzi wa vifaa tiba hadi kukamilika imeghalimu jumla ya shilingi 128,579,000/=
Wazo la kujenga Zahanati hii ilizingatia idadi ya wakazi wanaoishi Liwale Mjini ni kubwa na watu ambao wanahitaji huduma ya matibabu kwa mujibu wa ripoti ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ina jumla ya watu 91,380 ikiwa wanaume ni 44,027 na wanawake ni 47,353.
Idadi hiyo ni la eneo la mjini pekee ambalo linajumuisha kata 3 ambazo ni Likongowele,Nangando na Liwale Mjini ikiwa na jumla ya watu 21,724 ikiwa wanaume ni 10,101 na wanawake ni 11,623.
Mkuu wa wilaya akiweka jiwe la msingi la Zahana ya mkoyage
Jiwe la msingi la Zahanati lilowekwa na Mh.Ephraim Mmbaga mkuu wa wilaya ya LiwaleMkuu wa wilaya akiweka jiwe la msingi la Zahana ya mkoyage
Baada ya kuweka jiwe la msingi mkuu wa wilaya aliweza kupanmda mti nje ya Zahanati ya Mkoyage akiwe kama kumbukumbu
Mkuu wa wilaya akikamilisha upandaji mti kama kuweka kumbukumbu ambayo haitasaulika kwa mchango wake alioutoa ili kuweza kufanyikisha kukamilika kwa Zahanati hii
Zahanati ya Mkoyage ilioyoweka jiwe la msingi hapo jana na mkuu wa wilaya ya Liwale,Mh.Ephraim Mmbaga iliyopo katika kata ya Likongowele Liwale Mjini.Jengo hili lina jumala ya vyumba 9 ambavyo ni chumba cha mganga ,upasuaji mdogo na sindano,vyumba viwili vya mapumziko,vyumba viwili vya maabara,chumba cha dawa na ofisi.
Baadhi ya vifaa tiba zilivyopo kwenye Zahanati ya Mkoyage ikiwa imekamilika na jumatatu itaanza kutoa huduma rasmi.
Zahanati hii ya Mkoyage imeweza kutoa ajira kwa hudumu wa Afya watu 16 kama wanapoonekana hapo juu.
Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ambaye ni mwenyekiti wa wa kamati ya Maandalizi ndugu Abbas Matulilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale ndugu Gaudence O. Nyamwihura akimpongeza mmiliki ya zahanati Bwana Musa Mkoyage pamoja wa wanaliwale kwa kuweza kuwekeza katika sekta ya Afya kwa kuweza kuongeza idadi ya zahanati na sasa kufikia zahanati 32 kati ya idadi hiyo Zahanati za serikali ni 30 na mbili za watu binafisi.
Katika wilaya ya Liwale kuna jumla ya vijiji 76 na kuna jumla ya idadi ya vituo vya Afya 30 tu kuna upungufu wa Zahanati 46.
Mgeni Rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Liwale,mh.Ephraim Mmbaga (Picha na habari na Liwale Blog)
Mkuu wa wilaya mh.Ephraim Mmbaga akikabizi kadi 15 za bima za afya kwa walemavu zitawawezesha kutiwa bure kwa mwaka 1 katika zahanati ya Mkoyage.
Wakazi wa Liwale wameshauri kuanza kuwekeza nyumbani ili kuweza kuwahamasisha wanaliwale na watu wengine kuvutiwa Liwale na kuacha kubeza kama Liwale hakuna Maendeleo yeyote yaliyofanyika.
Hayo aliyasema Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Liwale,Mh.Ephraim Mmbaga kwenye uwekaji wa jiwe la Msingi ya Zanahanati ya Mkoyage hapo jana iliyopo katika kata ya Likongowele wilayani Liwale mkoani Lindi.
Mmbaga alimshukuru mmiliki wa Zahanati hiyo kwa kuweza kuanza kuwekeza nyumbani katika sekta ya Afya pia alisema huu ni mfano wa kuigwa kwa wanafanyabishara mbalimbali waliopo katika wilaya ya Liwale.
Katika uzinduzi huo Mmbga amempongeza Bwana Musa Mkoyage ambaye ni mmiliki wa Zahanati kwa kuweza kuwajali watu wenye ulemavu 16 kwa kuwapa kadi za bima za afya kuweza kutibiwa matibu BURE katika Zahanati hiyo ndani ya mwaka mmoja.
Nae mbunge alimaliza muda wake katika jimbo la Liwale Mh.Faith Mitambo aliweza kutoa zawadi ya Hadubini (Microscope) yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000/=) kwa Bwana Mkoyage ikiwa moja ya uungaji mkono wake katika kuweza kutoa huduma bora katika wilaya hiyo na alisema atamuunga mkono kwa mtu yoyote bila kubagua katika suala ya kimaendeleo.
Bwana Musa Mkoyage aliwashukuru wadau wote waliomweza kukamilisha Zahanati hiyo ikiwemo Mkuu wa wilaya,Meneja wa Banki ya NMB tawi la Liwale,Mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya,idara ya ujenzi na wadau mbalimbali.
Wizara ya Afya katika malengo yake Kitaifa ,imelenga kuimarisha huduma bora za Afya kupitia mpango wa PPP(PUBLIC PRIVATE PERTNERSHIP) ikimaanisha utoaji wa huduma kwa ushirikiano na wadau wa sekta binafsi hiyo ndio uwepo wa Zahanati hii ni ushirikiano wa kisekta.
Uwezo wa Zahanati alisema kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wa nje yaani "Out Patient" ikiendana na huduma ya mapumziko mafupi kwa wagonjwa wawili kwa mara moja kwa wale wagonjwa ambao hali zao zitaonekana zinahitaji mapunziko ya muda.
Kituo hiki kina jumla ya watoa huduma wa Afya 14 ikiwa madaktari 3,wauguzi 7,wataalam wa maabara 4,mlinzi mmoja na mhudumu wa ofisi mmoja sawa na jumla ya watumishi 16.Pia kituo kina uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa takribani 45 kwa siku ambao wanakadiriwa kuhudumiwa na madaktari hao idadi hii ya wagonjwa imetokana na uwiano wa kila Daktari mmoja kuhudumia wagonjwa 15.
"Natumia nafasi hii niwaombe radhi kwa wale ndugu zangu waliokosa nafasi hii ya ajira hapa wanaosema kwanini mtoto wangu hakuwepo hapa mimi mtoto wangu anaendesha Powertila ningependa hawe hapa lakini hana talaamu hiyo nimeheshimu ushauri wa serikali pamoja na sheria kwa kuwaweka wenye talaamu"alisema Mkoyage.
pia aliongeza kusema kutakuwa na huduma za upimaji wa magonjwa zitakazopatikana katika kiwango cha kuridhisha na zahanati ina kitengo cha utoaji wa dawa kulingana na kiwango kilichorusiwa na wizara ya Afya kwa kuata Mwongozo wa Wizara ya Afya mara kituo kitakapokamilisha usaji katika mfuko wa Bima ya Afya kinalenga kutoa huduma za afya kwa wananchi wanaotumia kadi za Bima afya ya Taifa "NHIF".
Mkoyage ameiomba serikali iharakishe usajili ili kuweza utoaji wa huduma hiyo ya NHIF.
Baadhi ya watu walioudhulia uwekaji wa jiwe hilo la msingi kwa niaba ya chama cha Wafanyabiashari ndugu Saidi Mautanga alisema watu wenye kipato na wadau mbalimbali waendelee kujitokeza katika uwekezaji katika sekta mbalimbali kwani mji wa Liwale kwa sasa unakuwa na unahitaji wa huduma mbalimbali.
Post a Comment