0

mchezo wa leo kati ya Bodaboda Vs Wakaanga Sumu mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano Liwale Mjini

Ligi ya Mbuzi Vijana CUP ilianza rasmi kutimua vumbi April 25 kukiwa na jumla ya timu 12 zinazoshiriki miongoni mwa timu hizo ni Z.F.C,SIDO FC,LIKONGOWELE,BODABODA,NANGANDO,KOMBAINI,VIJUSO,MNALANI,KIGAMBANI,
KUBOTA,WAKAANGA SUMU NA BLACK STAR

Leo april 28 mashindano yaliendelea tena wilayani Liwale mkoani Lindi leo ikiwa ni siku ya tatu ya mashindano ya mpigara wa miguu,kulikuwa na mchezo kati ya Bodaboda Vs Wakaanga Sumu mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano Liwale mjini.

Timu ya Bodaboda iliweza kuibuka na ushindi wa goli 4 kwa 1 katika kipindi cha kwanza timu ya Bodaboda ilikuwa ndio ya kwanza kujipatia goli la kwanza la kuongoza namo dk ya 25  huku timu ya Wakaanga Sumu waliweza kusawazisha goli katika dakika ya 30 mpaka mapunziko timu zote zilikuwa zimefungana goli moja kwa  moja
Katika kipindi cha pili timu ya Bodaboda ilifanyikiwa kuongeza goli 3 huku ikikosa penaiti iliyopigwa na mchezaji anayefahamika Badi

Kesho April 29 kutakuwa na mchezo kati ya Nangando Vs Kombaini

MATOKEO YA MICHEZO ZILIZOPITA
APRIL 25 Z.F.C 1-6 MNALANI
APRIL 26 SIDO 1-1 KUBOTA
APRIL 27 LIKONGOWELE 1-3 KIGAMBONI
APRIL 28 BODABODA 4-1 WAKAANGA SUMU

Post a Comment

 
Top