Lightsey alihitaji trekta kumbeba mamba huyo. Mamba huyo anaonekana hapa na mwanawe Lightsey, Mason
Mwindaji Lee Lightsey amesema mamba huyo wa ukubwa wa futi 15 (4.5m) ndiye mkubwa zaidi ambaye amekumbana naye katika kipindi cha miaka 18.
Baada ya kumuua, alihitaji trekta kumbeba.
Bw Lightsey alimgundua mnyama huyo akiwa na mwelekezi wa wawindaji Blake Godwin walipokuwa katika maeneo ya kumnyweshea mifugo maji Jumamosi.
Walimfyatulia risasi mamba huyo alipokuwa umbali wa mita sita kutoka kwao.
"Ingawa mnyama huyu ni mnene hivi, sijashangaa kwamba amekuwepo,” amesema Bw Lightsey.
- Je wajua siri ya Mamba usingizini?
- Mamba kulinda wafungwa hatari Indonesia
- Kwa Picha: Ndovu dhidi ya mamba
"Kilichotuvutia ni kwamba anaonekana amekuwa akiwala ng’ombe wetu, kwa sababu tulipata vipande vya nyama majini. Alikuwa dubwana lililostahili kuangamizwa.”
Bw Lightsey anasema mamba mkubwa zaidi ambaye amewahi kumuua alikuwa na urefu wa futi 13ft (4m).
Eneo la kusini mwa Florida ndilo pekee ambalo mamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi kwa pamoja.
Bw Lightsey amesema anapanga kumhifadhi mamba huyo lakini nyama yake ataikabidhi kwa wahisani.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.