Gari
la Mizigo lililokuwa linasafirisha shehena ya bidhaa mbalimbali kutoka
Dar es Salaam kwenda nchini Zambia limeungua kwa moto baada ya kutokea
hitilafu ya kiufundi katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro
na bidhaa zote zilizokuwa ndani ya Gari hilo zimeteketea na hakuna mali
iliyookolewa.
Akiongea na itv katika mji mdogo wa Mikumi Mkoani Morogoro Dereva
wa Gari hilo la mizigo Francis Semkiwa amesema gari hilo lilipata
hitilafu ya ghafla usiku wa kuamkia jana baada ya kupita kwenye matuta
ya barabarani katika hifadhi hiyo na ilianza kuwaka moto ambao
umeteketeza mali zote ikiwemo nguo aina ya mitumba na viatu vilivyokuwa
kwenye gari hilo lenye namba za usajili T 806 DEP lakini watu wote
watatu waliokuwemo kwenye gari hilo wamenusurika na ajali hiyo.
Kwa upande wake Msemaji wa Kampuni inayomiliki gari hiyo ya
jijijini Dar es Salaam Gelan Hamad amewashukuru wadau mbalimbali ikiwemo
Jeshi la Polisi na hifadhi ya taifa ya Mikumi kwa ushirikiano walioutoa
wakati wa tukio na kwamba mawasiliano na mteja wao mmiliki wa mali
zilizoteketea aliyeko Ndola nchini Zambia yanaendelea.
Kutokana na ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara katikati
ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kusababisha uharibifu wa mali na
miundombinu ikiwemo ile ya gari lililogonga na kuua nyati wanane, baadhi
ya wadau wa uhifadhi wamekuwa wakishauri serikali kuridhia mpango wa
barabara hiyo kuhamishwa na kupita wilayani kilosa ili kuepuka matukio
ya ajali na vifo vya watu na wanyamapori na pia uharibifu wa mali lakini
pia utalii wa bure na uchafuzi wa mazingira
Post a Comment