
Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA Harry Kitilya na Bi.Shose Sinare,Siyoi Abraham Solomon wamefikishwa Na TAKUKURU katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kushtakiwa kwa makosa nane, ikiwemo utakatishaji fedha.

Aliyekuwa Kamishina Mkuu wa mamlaka
ya mapato nchini TRA Harry Kitilya na wenzake wawili akiwemo aliyewahi
kuwa miss Tanzania Bi Shose Sinare wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka nane likiwemo
la kutakatisha fedha haramu.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi
Emilius Mchauru ambapo Wakili Mkuu wa Serikali Oswald Tibabyekomya
amsema kati ya mashataka hayo nane Bi Sinare Kanaliwa ana mashtaka yote
nane wakati wenzake wakabiliwa na mashtaka manne miongozi mwa mashtaka
hayo.
Inadiwa kuwa kati ya August 2012 na March 2013 katika jiji la Dar
es Salaam washitkiwa hao wote kwa pamoja walikula njama ya kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka katika Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Aidha watuhumiwa hao tarehe 5 Novemba 2012 katika Benki ya
Stanbic makao makuu yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam
walitengeneza mkataba wa kughushi kuonyesha kuwa kampuni ya EGMA
itaratibu upatikana wa mkopo wa dola za kimarekani milioni 550 kutoka
Standard Bank ya London kwa kushirikiana na Stanbic ya Tanzania na
kisha wao wangejilipa asilimi 2.4 ya fedha hizo.
katika shtaka lingine watuhumiwa hao wote kwa pamoja kati ya March
2013 na Septemba 2015 jijini dar es Salaam walitakatisha fedha dola
za kimarekani milioni sita kwa kuzihamisha kutoka katika Account za
EGMA zilizokuwa zimefunguliwa Stanbic Tanzania kwa namba mbalimbali
na kisha kuzihamishia katika akaunti za benki zingine kama KCB
wakijuwa kuwa fedha hizo hazikuwa safi badaa ya kusomewa mashtaka hayo
uliibuka mvutano wa kisheria kama wanaweza kupewa dhamana au laa hatua
ambayo Hakimu anayendesha shauri hilo amesema atalitolea uamuzi ijumaa
ijayo na hivyo washtakiwa wamekwenda rumande.
katika kesi nyingine Mbunge wa Sumve Mh.Richard Ndasa amepandishwa
katika kizimba cha mahakama hiyo mbele ya hakimu huyo akikabiliwa na
mashtaka mawili ikiwemo kujihusisha na vitendo vya rushwa ya shilingili
milioni 30.
Post a Comment