Wabunge
wamevitaka vyombo vya kuichunguzi kuhakikisha vinazifanyia kazi tuhuma
za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge kwani ni dhahiri zinashusha
hadhi ya Bunge na kuwafanya wananchi kutokuwa na imani na wawakilishi
wao.
Katika mahojiano maalum na ITV kwa nyakati tofauti jijini Dar es
Salaam wabunge hao kutoka majimbo ya Mtera,Nyamagana,Magomeni Visiwani
Zanzibar wamesema uwepo wa tuhuma hizo kwa wabunge waliopewa dhamana
kubwa ni fedheha kwa Bunge, huku wakitaka hatua stahiki kuchukuliwa kama
tuhuma hizo zitabainika.
Maafisa wa Bunge wanasema moja ya hatua za awali waliokwisha
kuzichukua ni pamoja na kuwavua uwenyeviti wa kamati za kudumu za bunge
wanaotajwa katika tuhuma hizo pamoja na kuwahamisha baadhi ya wabunge
kutoka kamati moja hadi nyingine,nakuahidi hatua nyingine zaidi
zitafuata.
Miongoni mwa hatua zilizokwisha kuchukuliwa na Spika wa Bunge chini
ya kanuni ya 116(3) cha kanuni za kudumu za Bunge,ni pamoja na kufanya
mabadiliko katika kamati 5 za Bunge pamoja na kufanya mabadiliko ya
wajumbe katika kamati hizo.
Post a Comment