Serikali
imewasimamisha kazi Maafisa 3 wa Jeshi la Kikosi cha Zimamoto kwa
tuhuma za kushiriki wizi wa mafuta ya Ndege na mmoja kati yao kuiba
mizigo ya wateja kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kampuni ya
Swissport.
Akizungumza katika Ziara ya kushitukiza aliyoifanya katika Viwanja
vya Ndege vya Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa
mambo ya ndani Mh.Mhandisi Hamad Masauni amewataja walio simamishwa kazi
ni Khalfani Kisana na Mussa Mandauli ambao walikamatwa na madumu 10 ya
mafuta ya Ndege wakiwa na gari la Serikali lenye usajiri STJ 2948 huku
askari mwingine aliyejulikana kwa jina la Abas Mwanza akishutumiwa kwa
kosa la kushirikiana na mfanyakazi wa Swissport |Lucas Maganda kwa kosa
la kuiba mzigo wa abiria.
Akiwa katika kiwanja hicho Mh.Masauni amekagua utendaji kazi katika
idara ya Uhamiaji,Polisi na Jeshi la Zimamoto na kuagiza viongozi wa
idara hizo zilizopo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uaminifu na
yeyote atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Post a Comment