Kampuni
inayotarajiwa kufanikisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya
Tanga hadi nchini Uganda imesema iko tayari kuanza ujenzi huo.
Makamu wa
Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw Javier Rielo amemwambia
Rais wa Tanzania John Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi huo
haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.
Mradi huo
utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo
litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari
ya Tanga.
Utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Bw
Javier, akikutana na Rais Magufuli ikulu ya Dar es salaam, amesema
kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4
ambazo tayari zimeshaandaliwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Rais
Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi,
na kupendekeza muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo
upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.
Waziri wa
Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, Tanzania pia inatarajia
kunufaika zaidi na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta
zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania.
Amesema zikikamilika kwa mafanikio, inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
Makubaliano
ya kujengwa kwa bomba hilo yaliafikiwa wakati wa mkutano kati ya Rais
Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mapema mwezi huu.
|
Post a Comment