0

 UZINDUZI WA HUHUMA YA INTERNET YA 3G
Wateja wa Tigo waishio Wilayani Liwale mkoani Lindi sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 3G  inayopatikana kwa sasa na inawaweza wateja wao kuweza kuperuzi internet kwa uhakika ikilinganisha na hapo awali.

Msambazaji wa huduma za tigo wilayani Liwale bw. Idrisa Mradi alisema Wamefunga huduma ya 3G wilayani hapa na leo wanazindua rasmi kwa kuwa kampuni ya Tigo ilikuwa ya kwanza kutoa huduma ya Tigo ndio maana imendelea kuthamini wateja wao.

"sasa tumeleta promotion ya laini kwa wateja wapya pia smartphone kwa bei ya shilingi 99000 na modem za tigo ambazo linauzwa kwa bei nafuu na sasa tunatarajia kujenga minara katika kijiji cha mirui,Barikiwa,makata na Lilombe ndani ya mwaka huu"alisema Idrisa 

Pia alisema leo wameweza kuwapata wateja wapya waliosajiliwa 150 ambao wamejiunga na mtandao wa Tigo na alibainisha kuwa wameweza kuongeza kwa kujenga mnara mwingine katika kata ya Likongoweza wilayani Liwale ili kupanua huduma kwa kuwafikishia wateja wao huduma muhimu kwa maeneo yaliyokuwa hayapati mawasiliano vizuri sasa mnara huo hutaweza kuwafikia wateja wake wa kijiji cha Kichonda,Mbaya,Namtumbwa,Mikunya na maeneo jirani.
 Kwenye uzinduzi wa huduma ya internet ya 3G uliofanyika leo wilayani Liwale pia kuliambatana na Bonanza ya michezo mbalimbali iliyofanyika katika uwanja wa wilaya ya Liwale  
 Gari la Tigo likirusha matangazo yake kwenye uzinduzi wa huduma ya internet ya 3G
 Baadhi ya wahudumu wa kampuni ya Tigo wakitoa huduma mbalimbali kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa wilaya hii leo
 Ni moja ya vituo vya kutolea huduma za Tigo zilizosambaa kwenye uwanja wa wilaya ili kuweza kuwapatia wateja wao huduma mbalimbali
 Timu ya Liwale United iliyoshiriki katika bonanza la Tigo na  kuibuka na ushindi wa bao 2 kwa 1 dhidi ya watani wao timu ya Liwale Star  na kuibuka na zawaidi ya  MBUZI mchezo uliochezwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale hii leo
 Timu ya Liwale Star ilioshiriki kucheza Bonanza lililodhaminiwa na kampuni ya Tigo lakini Timu hii iliweza kufungwa bao 2 kwa 1 dhidi ya wapinzani wao Liwale United
 Mashabiki waliokuja kuangalia burudani mbalimbali zilizoandaliwa na Kampuni ya Tigo katika uzinduzi wa huduma ya internet ya 3G iliyofanyika katika uwanja wa wilaya

 mchezo uliovutiwa na mashabiki wengi na kuweza kuburudika kwa namna moja





Wachezaji wakioneshana ufundi wa jinsi ya kumtoroka adai ukiwa na mpira

 Timu ya Liwale United ikishangilia ushidi mara baada ya kuifunga timu ya Liwale stars
 Kocha wa timu ya Liwale United, bw.Juma Kamkosa alisema anashurukuwa kwa kuweza kuwafunga wapinzaji wao na anakuwa anaendelea kuwafunga.

Nae nahodha wa timu ya Liwale Star,Leman Mtipa alisema hali ya mchezo ulikuwa mgumu sana na tatizo la kufungwa ni ukosefu wa mabeki katika timu yake

.Mbuzi akiwa amenjanyuliwa juu mara baada ya kukabiziwa zawaidi yao kwa kuweza kushinda

Post a Comment

 
Top