
Awadh
Juma (mbele) akipongezwa na wachezaji wenzake Mussa Mgosi (kulia) na
Danny Lyanga (kushoto) baada ya kuifunga bao lililoipa Simba pointi
tatu.

Wachezaji wa Simba wakimlaki Awadh Juma baada ya kufunga bao na
kuihakikishia timu yake kupata pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi
ya TZ Prisons
Dar es Salaam
Wakati watani zao wa jadi Yanga wamemaliza kucheza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili katika michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda kwa ushindi wa goli 2-1 March 12, Simba wao wameshuka dimbani March 13 kuendeleza harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.Simba wameshuka dimbani kucheza dhidi ya klabu ya wajelajela wa Mbeya Tanzania Prisons, katika mchezo wao 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara. Simba waliingia uwanjani kuhakikisha wanapata point tatu ili waendelee kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Hata hivyo licha ya jitihada kubwa kuoneshwa ndani ya dimba la uwanja wa Taifa na Tanzania Prisons za kuataka kutoa sare, hazikuzaa matunda, kwani Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 kupitia kwa Awadh Juma dakika ya 88.
Kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi akiwa na jumla ya point 54 akifutiwa na Yanga aliyemzidi point 3 na michezo miwili.
MATOKEO YA MECHI ZA LEO MARCH 13 VIWANJA VINGINE
Majimaji 1-0 Stand United
Kagera Sugar 3-0 Coastal Union
Mgambo JKT 1-1 Mwadui FC
MSIMAMO WA LIGI YA VODACOM PREMIER LEAGUE
| Name | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | |||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Simba SC | 23 | 17 | 3 | 3 | 41 | 13 | 28 | 54 | |||
| Young Africans | 21 | 15 | 5 | 1 | 51 | 11 | 40 | 50 | |||
| Azam FC | 20 | 14 | 5 | 1 | 36 | 13 | 23 | 47 | |||
| Mtibwa Sugar | 21 | 11 | 6 | 4 | 26 | 14 | 12 | 39 | |||
| Tanzania Prisons | 23 | 9 | 9 | 5 | 21 | 20 | 1 | 36 | |||
| Mwadui FC | 23 | 9 | 7 | 7 | 22 | 19 | 3 | 34 | |||
| Stand United | 22 | 9 | 3 | 10 | 19 | 20 | -1 | 30 | |||
| Ndanda FC | 22 | 5 | 9 | 8 | 19 | 23 | -4 | 24 | |||
| Mbeya City | 22 | 6 | 6 | 10 | 22 | 28 | -6 | 24 | |||
| Majimaji | 23 | 6 | 6 | 11 | 13 | 32 | -19 | 24 | |||
| Toto Africans | 22 | 5 | 8 | 9 | 19 | 30 | -11 | 23 | |||
| Kagera Sugar | 23 | 5 | 7 | 11 | 16 | 25 | -9 | 22 | |||
| JKT Ruvu | 23 | 5 | 6 | 12 | 23 | 37 | -14 | 21 | |||
| Mgambo JKT | 23 | 4 | 8 | 11 | 18 | 28 | -10 | 20 | |||
| Coastal Union | 23 | 4 | 7 | 12 | 14 | 28 | -14 | 19 | |||
| African Sports | 22 | 4 | 5 | 13 | 7 | 26 | -19 | 17 | |||
Post a Comment