HATIMAYE
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imekisikia kilio
cha muda mrefu cha Wananchi ambao walikuwa wakilalamika kupanda kwa
bei ya sukari nchini.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mchana huu jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Semwaza amesema kuanzia sasa
kilo moja ya sukari itauzwa kwa sh. 1800 nchi nzima.
“Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja. “Amesema Semwaza na kuongeza;
” Wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi.
“Maafisa
biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa
agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki
za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo. “
AGIZO LA SERIKALI KUHUSU BEI ELEKEZI YA SUKARI
Post a Comment