Ashley Guindon
Polisi mmoja wa kike nchini Marekani amepigwa risasi na kuuawa katika siku yake ya kwanza kazini.
Askari
huyo bi Ashley Guindon alikula kiapo mapema siku hiyo hiyo kisha
akaelekezwa na wakubwa wake kwenda nyumbani kwa mama mmoja kutatua mzozo
wa kinyumbani katika kitongoji Washington, DC.Bi Ashley akiandamana na wenzake wawili walikwenda Woodbridge, Virginia, kilomita 32 kusini mwa Washington lakini walipofika huko walifyatuliwa risasi na kwa bahati mbaya Ashley hakubahatika.
Wenzake wawili pia walijeruhiwa vibaya na wamelazwa hospitalini.
Mwanjeshi huyo alikamatwa baadaye na vitengo maalum vya polisi.
Mwanjeshi huyo alikuwa amempiga risasi na kumuua mkewe papo hapo kabla ya Ashley na wenzake kutokea.
Hakukuwa na mtoto nyumbani wakati wa ufyatulianaji huo wa risasi.
Afisa mkuu wa kituo " Tunasikitika kuwatangazia kifo cha afisa wa polisi wa kituo cha Prince William County bi,Ashley Guindon, aliaga dunia kufuatia ufyatulianaji risasi katika mtaa wa Lashmere Ct akiwa kazini.
''Tunafurahi kuwakaribisha afande Ashley Guindon na mwenzake kwa huduma kwa wote''
Post a Comment