0
Mh. Mwigulu Nchemba
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Ubelgiji nchini Bwana Paul Cartier na kulia kwa Balozi ni Afisa kutoka Ubalozi huo Bibi. Isabelle Wittoek 
(Picha Maktaba)

Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Imeelezwa kwamba, japokuwa sekta ya kilimo nchini inatoa 95% ya mahitaji ya chakula, na kuchangia 30% ya mauzo ya nje. Lakini bado mfumo wa masoko uliopo unachangamoto kubwa.

Hayo yalielezwa jana mjini Lindi, na meneja mahusiano wa mamlaka ya masoko, dhamana na mitaji, Charles Shirima, wakati wa mafunzo ya uanzishwaji wa soko la bidhaa, ikiwamo za kilimo.

Shirima ambae alikuwa ni miongoni mwa watoa mada katika mafunzo hayo, alisema pamoja na juhudi za kuboresha mfumo wa masoko zinazofanywa na serikali, bado kunachangamoto kubwa.

Kwasababu mfumo uliopo haujakidhi ipasavyo mahitaji ya masoko ya mazao ya kilimo. Meneja huyo alisema mfumo wa soko bado umehodhiwa na wanunuzi wachache ambao wamekuwa wakipanga bei za kununulia mazao, hivyo kusababisha kukosekana ushindani.

Alisema mfumo wa masoko uliopo hautabiriki na matatizo mengi, ikiwemo wanunuzi kufanya migomo ya kununua mazao ya wakulima wakati serikali inapoingilia kati kwa kutoa bei elekezi ili kuwasaidia wakulima wasidhulumiwe.
"Vilevile taarifa za masoko, hususani bei na kiasi kilichouzwa na kununuliwa bidhaa zilizopo sokoni zimekuwa hazitolewi kwa wakati na uwazi kwa wakulima wote," alisema Shirima.

Kwa upande wake, katibu tawala wa mkoa wa Lindi, Ramadhani Kaswa, elimu kuhusu masoko haina budi kufikishwa kwa wakulima wa vijijini, ili kuwanusuru wasinyanyaswe na kupunjwa na wajanja wachache ambao hawavuji jasho kama wakulima hao.

Pia alitoa wito kwa vyama vikuu vya ushirika vilivyopo katika mkoa huu kuyatambua mazao mengine ya kilimo yanayolimwa katika mkoa huu, badala ya kutegemea korosho na ufuta pekee.

Nae meya wa manispaa ya Lindi, Mohamed Liumbo, alisema pamoja na mfumo mzuri wa stakabadhi za mazao ghalani, lakini wakulima wanakero nyingi. Hivyo kunahaja ya viongozi na watendaji kuepuka kasoro zinazotokana na uzembe.

Hivyo kuna haja kwa viongozi na watendaji hao wa serikali, kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza na kutekeza wajibu wake kikamilifu, ili sekta ya kilimo iwe natija kwa wakulima na taifa.

Post a Comment

 
Top