The Airlander 10 ina urefu wa mita 92 ikiwa ni mita 18 zaidi ya urefu wa ndege ya kawaida.
Picha mpya za ndege ndefu zaidi duniani zimetolewa kabla ya kuzinduliwa kwa mara ya kwanza.
Ndege hiyo inayojulikana kama (The Airlander 10) ina urefu wa mita 92 ikiwa ni mita 18 zaidi ya urefu wa ndege ya kawaida.Itaondolewa kwenye kiwanda hicho kwa mara ya kwanza tangu ujenzi wake ukamilike siku ya Jumatatu.
Jeshi la Uingereza liliishiwa na pesa za kumaliza ujenzi wake kuitumia kama ndege yao ya ujasusi hali iliyosababisha kampuni ya huduma za ndege ya Uingereza kujitwika jukumu la kuikamilisha.
Wengi wanaamini kuwa ndege hiyo isiyo na kelele ikiwa angani wa isiyotoa hewa chafu inaweza kutumiwa kwa usafiri siku za usoni.
Post a Comment