Waziri
wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi
Mkurugenzi msimamizi wa wanyamapori Dkt.Charles Mulokozi kupisha
uchunguzi kwa tuhuma za kuhusika kutoa vibali vya kusafirisha Tumbili 61
kupitia uwanja wa ndege wa kimatifa ya Kilimanjaro-KIA- kwenda Albania
kinyume cha taratibu.
Uamuzi huo wa Profesa.Jumanne Maghembe umetokana na jeshi la Polisi
kukamata rai wa wawili wa Uholanzi katika uwanja wa ndege wa KIA wakiwa
katika ndege ya kukodi ya Afrika Kusini wakiwa na Tumbili 61 wakijaribu
kuwasafirisha kuelekea nchini Alabinia huku zaidi ya Tumbili 450 wakiwa
wamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali nchini wakiwa katika mpango wa
kusafirishwa kuelekea nchini humo.
Aidha Profesa.Maghembe amewasimamisha kazi kupisha uchunguzi
viongozi waandamizi sita akiwemo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa huduma za
misitu Tanzania Bwana. Juma Mgoo,Mkurugenzi wa rasilimali Misitu
Bi.Zawadi Mbwambo,Mkurugenzi wa matumizi ya rasilimali misitu pamoja na
Mkurugenzi wa biashara na huduma Bwana Emmanuel Wilfred pamoja na
baadhi ya mameneja wa kanda kutokana na kukamatwa magogo yenye thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 500 wilayani Karambo Yakiwa katika mpango
wa kusafirishwa kwenda nchni china.
Post a Comment