0


 wananchi wakiwa kwenye mkutano wakisikiliza kwa umakini mambo muhimu kutoka kwa viongozi mbalimbali
wananchi wakiwa kwenye mkutano wakisikiliza kwa umakini mambo muhimu kutoka kwa viongozi mbalimbali
Mbunge wa jimbo la Liwale mh.Zuberi Kuchauka akiongea na wananchi na kuchukua kero mbalimbali ili kuweza kupeleka bungeni


NA Mwandae Mchungulike,Liwale
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Liwale bwana Mohamedi Mtesa amewashukuru wanachi kwa kuweza kuwachagua viongozi makini watakao weza kufanya kazi za kimaendeleo walizotumwa na wananchi. 

Hayo aliyasema jana kwenye mkutano ulifanyika katika kata ya Nangando tarafa ya Liwale mjini mkoani Lindi.

“Ndugu zangu mumetupa kazi tatu za kufanya na sisi kazi za kufanya tunazijua kazi ya kwanza kutetea haki zenu,kusimamia uwepo wa maendeleo katika halmashauri yetu na kuhakikisha usalama wa wananchi tumeanza nayo na tunayafanyia kazi pia napenda kuwaambia kuwa mchango wa kukatwa shilingi 30 kwa kilo za mazao sasa umefutwa  tunajua sisi Halmashauri tunaumia ila kwakuwa mulikatwa kwa muda mrefu sasa tunabalansi”alisema Mtesa.

Mtesa alisema maliasili imekuwa  mwiba kwa wananchi wa wilaya ya Liwale amewaomba kwa nia njema kama viongozi wa halmashauri jukumu la maliasili ni kulinda wanyama lakini pia wanahitaji ushirikiano wa ulinzi kutoka kwa wananchi lakini hawawezi kufanya kazi ya ufanisi bila ushirikiano wa wananchi.
Alisema mazao ya wakulima yanaliwa na Nguruwe ikitokea Nguruwe ameuwawa wananchi wanachukuliwa hatua kali ambayo haiendani na kosa  pia amewashauri maliasili wanatakiwa kuwa na busara kwa wananchi ili kuweza kupata ushirikiano na wananchi.

“Hatuhalalishi  ujangili kama kuna mtu anashughulika na ujangili tunamuomba aache sisi hatutawatetei ujangili sisi tunahitaji kujenga ila tunahitaji bao za milango kama jambo hili halitakuwa na mabadiliko hatawaunga mkono lakini yakitokea mabadiliko mazuri nitaungana nao kupita kijiji hadi kijiji kuwahamasisha wananchi kuwapa elimu sasa tunasubiri matokeo kama yatakuwa siyo na sisi tutasema siyo”alisema Mtesa.

Mtesa alisema watu wafanye kazi kwa bidii ili watu wajiongezee kipato jambo kubwa la kufanya kazi kwa kujituma halmashauri imekuja na mkakati wa kuwahamasisha wananchi kuongeza zao mbadala la biashara la arizeti kwani ardhi ya Liwale inastawi mahali popote hatuwezi kuendelea kutegemea mazao ya korosho na ufuta tu lazima tuongeze zao jingine ili kipato kiongezeke.

Tatizo la viwanja  watu wamepewa viwanja lakini watu wamekaa kimya hawajavilipia mpaka sasa Mtesa alibainisha  kuwa kama wananchi  waliopewa viwanja  inakuwa tatizo kulipia kwa wakati ,walipopewa viwanja waliambiwa baada ya siku 21 wawe wametanguliza kutoa shilingi laki mmoja (100,000/=) kwa kiasi cha thamani ya kiwanja alichopewa lakini watu wameshindwa kulipia  hata shilingi toka septemba mwaka 2015 watu wa aina hii hawatavumiliwa kwani watu wengine wanahitaji viwanja pia  ili kuweza kumaliza tatizo la viwanja kwa watu wanaodai toka mwaka 2009.

 Kwa upande wake mbunge wa Liwale Mh.Zuberi Kuchauka  alianza kwa kuwashukuru wananchi wakati anaomba ridhaa kwa kupita kila kijiji aliwahaidi wananchi kuwa yeye atakuwa sauti  kwa waliokosa  sauti na atakuwa mwakilishi kwa waliokosa  mwakilishi na kusema kuwa kwa sasa muda wa kufanya siasa  umekwisha bali  yeye ni mbunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na si mbunge wa chama kimoja au watu wachache  huku akisema kuwa yeye ni mpenda maendeleo hivyo kwa kushirikiana na wananchi walioko katika jimbo lake washirikiane kwa pamoja kufanya kazi kama sera ya muheshimiwa rais Magufuli inayosema [ hapa kazi tu].

Pia mheshimiwa Kuchauka akabainisha kuwa mara baada ya kuapishwa  kuwa mbunge akaanza na dhiara mbalimbali ikiwemo kutembelea katika sekta mbali mbali ikiwemo Mashirika  ya umma ,mashirika binafsi,na ikiwemo idara ya Kilimo ,Afya ,maliasili,maji Mahakama ,Polisi, huku akisema kuwa AFYA;kwa upande wa sekta ya afya bado huduma si mzuri na  hospitali ya wilaya ya Liwale haina hadhi ya kuitwa hospitali pia  anahitaji  kuepo kwa dhahanati kila kijiji hivyo amedai kuwa atapambana na hali hiyo huku akiweka kipaumbele kikubwa katika afya kwakuwa afya ndio kila kitu katika jamii na kuhaidi kutekeleza uwepo wa huduma mzuri kwa wakinamama wajawazito na watoto huku akisema amepeleka kapeti za kutosha pamoja na gloves huku akihaidi kupeleka ndoo na mabesen kwa ajili ya akinamama wajawazito.

Huku akisema kuwa  amefanya jitihada za kurekebisha mashine ya x-ray na sasa inafanya kazi pia amewaomba wana Liwale  wajiunge na mfuko wa bima ya afya wa  CHF ambao utawawezesha kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa shilingi alfu kumi kwa watu 6 kwa kila kaya na kusema yeye ameweza kuchangia kaya 100 na tayari amesha lipia kiasi cha shilingi million 1 huku akitoa  changamoto ya watu kutopata dawa mara baada ya matibabu hivyo amewataka wahusika kuwa makini katika huduma hiyo muhimu.

ELIMU;Mara baada ya kuhitimisha katika sekta  afya mheshimiwa aliongelea pia katika sekta ya Elimu na kusema kuwa bado hali ya ufaulu kwa shule za sekonali wilaya ya Liwale si mzuri huku akisema shule ya sekondari  liwale day tu ndiyo angalaau imeweza kutoa  division 1 tano tu kwa willaya mzima hivyo amewataka wazazi washirikiane na walimu katika kuhakikisha maendeleo ya wanafunzi yaweze kuwa mazuri pia amezungumzia upande wa elimu yamsingi na kusema kuwa kuna uhaba mkubwa wa walimu ,uhaba wa madarasa ,nyumba za walimu huku akiwataka wazazi wanaohamahama kwenda mashambani wahakikishe sehemu wanazohishi zinapatikana huduma zote za jamii ili kurahisisha watoto wao kupata elimu.

KILIMO;Pia katika sekta ya kilimo ameweza kubainisha changamoto kwa kusema kuwa watu wengi wamejisahau badala ya kulima mazao ya chakula wengi  hulima mazao ya biashara na kusema kuwa changamoto nyingine ni  kuwa maafisa ugani ni mizigo kwa baadhi ya maeneo ya vijijini kama Mpigamiti,kikukulyungu na mirui  ambayo huchangia wakulima kushindwa kufanya vizuri katika kilimo kwakuwa maafisa wengi wanakaa tu maofisini bila kuwatembelea wakulima huku akisema kuwa changamoto nyingine ni uwepo wa nguruwe ambao wanamaliza mazao na kusema kuwa ameshaenda maliasili mara tatu nakumtaka mkuu wa kitengo cha maliasilia atumie hekima ambayo itaweza kutatua tatizo hili na si kwa kuwapa fain kubwa  wakulima wanaoua nguruwe huku wanyama hao wanama liza mazao.

MGOGORO WA MPAKA;Kijiji cha kikulyungu na selous amesema shughuli za utalii zisimame kwa sababu eneo lile lina mgogoro lakini pia alizungumzia mgodi uliyoko lilombe na kukuta hakuna unufaikaji  wowote kwa wanakijiji ama halmashauli kutokana na uchimbaji unaoendelea katika eneo hilo bali wanaochimba katika eneo hilo huwa wanalipia nachingwea na kupata kibali huko hivyo hakuna manufaa yoyote kitika mgodi huo hiyo mheshimiwa mbunge amehaidi kufwatilia swala hilo ili kuhakikisha manufaa yanapatikana.

POLISI;mheshimiwa pia amebainisha ukosefu wa vituo vya polisi katika maeneo ambayo yanakuwa kimaendeleo na kibiashara katika wilaya ya liwale kama vile kijiji cha  Kibutuka na Lilombe na kuhaidi kujitahidi kufwatilia na kuhakikisha maeneo hayo nayo yanakuwa na vituo.

MAJI;Pia ametembelea maeneo mbalimbali ambayo yanachangamoto za maji na kusema kuwa tayari serikali ilikwisha toa million miambili ambazo ni za miundombinu ya maji wilayani liwale.

Pia akazungumzia swala la mahindi ambayo baadhi ya  watu wanamshutumu kuwa amemuuzia mahindi ambayo ni msaada wa wananchi liwale mfanyabiashara aliyoko wilayani hapo Bwana Amidu Wamo si sahihi na awezi kufanya kitu kama hicho bali kama mahindi ya serikali ambayo yanauzwa shilingi 150 kwa kilo hayo yamefikia katika halmashauri ya wilaya ya liwale na madiwani wote wanafahamu.

Post a Comment

 
Top