WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa alisema Tanzania inaweza kujitegemea kwa zaidi ya
asilimia 80 katika bajeti yake kutokana na vyanzo vyake vya ndani.
Amesema kutokana na rasilimali zilizopo, Tanzania inaweza kukidhi bajeti
yake kwa asilimia 80 bila kutegemea msaada kutoka nje na kwamba suala
la kukabiliana na ufisadi na ukwepaji kodi ni endelevu.
Waziri
Mkuu Majaliwa alisema hayo juzi mjini Lamadi wakati akihutubia maelfu
ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika siku ya kwanza ya ziara
yake ya siku sita mkoani Simiyu. “Tanzania inaweza kujitegemea kwa
asilimia 80 kwa mapato yake kutokana na rasilimali na vyanzo vyake vya
ndani.
Hili
linawezekana. Ndio maana tumeamua kubanana,” alieleza Waziri Mkuu.
Alisema ndio maana wameamua kupambana na ufisadi na ukwepaji kodi kwa
nia ya kuhakikisha wanapata fedha za kuwatumikia Watanzania kwa fedha za
ndani kupitia mapato yake.
Alisema
hata uamuzi wa kupitisha fedha zote katika Mfuko Mkuu wa Serikali
ulikuwa na nia ya kutambua mapato yake yote ili fedha hizo zikasaidie
kuleta maendeleo ikiwamo kuisimamia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili
kubana mianya yote ya ukwepaji kodi.
Alisema
hali hiyo imesaidia kwani mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 1.3
Desemba mwaka jana, Sh bilioni 1.5 Januari mwaka huu na mwezi uliopita,
alisema ana hakika zitavuka zaidi.
Alisema
kutokana na hali hiyo, serikali ndio maana inagharimia mambo yake mengi
likiwamo suala la elimu bure, na kwamba licha ya kuwapo kwa changamoto
mbalimbali, watahakikisha Watanzania wanapata huduma mbalimbali
zilizoboreshwa.
Aliyekuwa
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akiwasilisha bungeni mapendekezo ya
Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha
2015/16, Juni mwaka jana, alisema jitihada za kuongeza mapato zimelenga
kuisaidia Serikali kupunguza utegemezi wa bajeti ya Serikali kwa fedha
za wahisani.
Alisema
kiwango cha utegemezi kimepungua kutoka asilimia 24 mwaka 2004/05 hadi
asilimia 17 mwaka 2010/11. Alisema pia kwamba utegemezi huo umekuwa
ukipungua mwaka hadi mwaka. Mwaka 2015/16 ilitarajiwa upungue kwa
asilimia 6.4.
Kuhusu
suala la mipaka kati ya hifadhi na vijiji, Waziri Mkuu alisema
amekwishaagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamia suala hilo na
kuhakikisha wanaliangalia limalizike kwa busara.
Lakini
ameagiza wananchi hasa katika wilaya za Busega na Bariadi kutoingia
tena katika hifadhi ambako inadaiwa wanapokonywa ng’ombe wao na askari
wa Wanyamapori kwa kutozwa Sh milioni tano hadi 10.
Amewaonya
askari hao wa Wanyamapori kuacha tabia hiyo na kwamba mwananchi yeyote
mwenye taarifa za askari anayeshiriki vitendo hivyo, kupeleka jina lake
kwa vyombo husika.
|
Post a Comment