NAIBU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamisi
Kigwangalla amezindua chumba kipya cha kulaza wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalumu (ICU) katika jengo la Mwaisela, Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi
huo wa huduma bora, umetajwa kuwa ni njia ya kuelekea kuondokana na
kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Dk Kigwangallah
alisema ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa, serikali itaondoa huduma ya
kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu na ndiyo maana
inaendelea kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo ya taifa.
Alisema
huduma hiyo itatolewa kwa gharama nafuu kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Alisema wizara inaangalia vizuri jinsi ya kuondoa utaratibu huo wa
kupeleka wagonjwa nje. “Sasa muanze kujipanga hapa Muhimbili.
Endapo
kutakuwepo na mgonjwa anayetaka kwenda nje idara husika ndiyo
itampeleka baada ya kujiridhisha wao wameshindwa kumtibu. Hapa kazi tu
haya ndiyo mabadiliko ya kweli ya serikali ya awamu ya tano
tunayoyaleta. “
Tumeshaanza
kuweka utaratibu tunahama kutoka kupeleka wagonjwa nje tunawaleta
hapa,” alisema Naibu Waziri huyo. Alisema kila taasisi itakuwa na bajeti
yao, wao kama wizara watakuwa wanapanga bejeti ya kuhudumia kila idara.
“Sisi
tunataka kutoa lawama hiyo kwetu kama wizara ibaki kwenu hospitalini.
Tunaondoa siasa iliyozoeleka kuwa viongozi ndio wanaopeleka wagonjwa wao
nje,” alisema. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa
Lawrence Museru alieleza furaha yake kushuhudia uzinduzi wa upanuzi wa
huduma za tiba ya wagonjwa mahututi itakayokuwa ikifanyika hapo wadini
baada ya kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wake pamoja na kufungwa kwa
vifaa tiba vya kisasa.
Alisema
uongozi wa hospitali hiyo umesimamia uboreshaji wa huduma ya tiba ya
wagonjwa mahututi kwa upanuzi na uwekezaji wa vifaa vya kisasa katika
wadi hiyo ya Mwaisela kama vile mashine za kupumulia na vifaa vya
uchunguzi wa kihadubini kwa magonjwa ya tumbo na mapafu.
Pia
ultrasound ya kisasa inayochunguza mishipa ya damu, vitanda vya kisasa
kwa matumizi ya wagonjwa mahututi ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo
ya kitaalamu.
|
Post a Comment