|
POLISI
imesema ina taarifa juu ya kuibuka kwa makundi ya kihalifu nchini na
imejipanga kukabili wahusika. Aidha, Kamishna Operesheni na Mafunzo wa
Jeshi la Polisi, Nsato Marijani, amehadharisha askari na watendaji wa
jeshi hilo, aliowataja kuwa wasaliti na kusema watakaobainika
watafukuzwa na si kuhamishwa vituo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu mikakati ya
jeshi katika mapambano ya uhalifu nchini, Marijani amewataka wananchi
kuwa watulivu , kutotaharuki kwa kile alichosisitiza kuwa nchi iko
salama wakati Polisi ikiendelea kujipanga kukabili vikundi husika.
Kamishna
Marijani alisema makundi ya uhalifu yanayoibuka nchini yamekuwa kero .
Alisema juhudi za makusudi zinafanywa kuyadhibiti kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
“Hatuwezi
kuweka mikakati yetu hadharani ya kukabiliana na vikundi vya uhalifu
vilivyoibuka hivi sasa, ila wafahamu kwamba tutawadhibiti kikamilifu,”
alisema Kamishna Marijani. Alisema hakuna haja ya wananchi kuwa na hofu
bali wawe watulivu na kuendelea kufanya shughuli zao za uzalishaji mali,
kwa sababu vyombo vya usalama vipo na vitahakikisha ulinzi na usalama
wa raia na mali zao unalindwa .
Alisisitiza
kwamba, ni vyema kwa raia wanapoona tabia au mienendo yenye mashaka ya
watu, watoe taarifa Polisi. Polisi wasaliti Akizungumzia suala la
nidhamu kwa askari na watendaji wa jeshi hilo, Kamishna Marijani alisema
watendaji wengi wa jeshi hilo wana nidhamu na wanafanya kazi kwa
weledi.
Hata
hivyo, alisema wapo wachache wanaochafua jeshi hilo. Alisema
watakapobainika, hawatawavumilia wala kuwahamisha vituo vya kazi, bali
watafukuzwa. “Watendaji wetu wengi wana nidhamu, ila wapo wachache
wanaotuchafua, kuanzia sasa hatutawahamisha vituo vya kazi,
tutawafukuza, kama walizoea huko nyuma , sio zama hizi, wajue kila zama
zina vitabu vyake”, alisisitiza .
Alisema
hatua hiyo wataitekeleza bila uoga wala kificho . Aliwataka wananchi
kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kuhusu taarifa za watumishi wa jeshi
hilo wasio na maadili ili hatua zichukuliwe.
Hivi
karibuni, kumejitokeza matukio kadhaa ya uhalifu hususan jijini Dar es
Salaam. Miongoni mwa matukio hayo, ni uvamizi wa benki ya DCB katika
eneo la Chanika, wilayani Ilala. Uvamizi mwingine ulifanyika Benki ya
Access , Tawi la Mbagala.
Post a Comment