0

Sehemu ya Pili
Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais

Ibara ya : 39 
(1) Kutakuwa na Makamo Wawili wa Rais ambao watajulikana kama Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.

(2) Ndani ya siku saba mara baada ya kushika madaraka, Rais atateua Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.

(3) Makamo wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais. Isipokuwa kwamba:
(i) iwapo chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais kimepata chini ya asilimia kumi (10) ya kura zote za Uchaguzi wa Rais, au
(ii) endapo Rais atakuwa hana mpinzani, basi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais itapewa chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi.

Matokeo ya Uchaguzi..

Post a Comment

 
Top