Kombe la dunia la Afrika Kusini
Maafisa wa Afrika Kusini wamesisitiza kuwa hawakulipa hongo.
Fifa inajaribu kukomboa makumi ya mamilioni ya fedha zilizochukuliwa kinyume cha sheria na wanachama wa shirikisho hilo pamoja na mashirika mengine ya soka.
Maafisa wa zamani wa shirikisho hilo Chuck Blazer na Jack Warner pamoja na Jeffery Webb ni miongoni mwa wale waliofunguliwa mashtaka na Fifa ambayo imewasilisha stakhabadhi kwa mamlaka ya Marekani.
Fifa imekuwa katika mgogoro tangu madai ya ufisadi kugunduliwa mnamo mwezi Mei 2015.
Kwa jumla watu 41 pamoja na kampuni kadhaa zimeshtakiwa na mamlaka ya Marekani.
Uchunguzi wa Marekani ulifichua ufisadi mkubwa katika shirikisho hilo na Fifa inakadiria kwamba mamilioni ya madola yaliibwa kupitia hongo,kiinua mgongo na mipango ya ufisadi iliofanywa na washtakiwa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.