Na. Ahmad Mmow, Kilwa.
Watalamu wa Afya Wilayani Kilwa wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na utumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao.
Njwayo
alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika kijiji cha Miteja
baada ya kuweka jiwe la msingi nyumba mganga wa zahanati ya kijiji
hicho, iliyojengwa kupitia mfuko wa Rais wa maendeleo ya jamii(TASAF).
Alisema
miongoni mwa mambo yanayosababisha malalamiko kwa wananchi ni baadhi ya
watumishi wa umma ikiwamo wa idara ya afya kufanya kazi kwa mazoea
kwakutozingatia maadili ya taaluma zao na utumishi wa umma.
Huku baadhi yao wakikosa uadilifu kwa kuiba mali na vifaa vya umma, ikiwamo dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali.
"Baadhi
ya wakunga mnakiuka maadili ya taaluma yenu na kusababisha akina mama
wajawazito kuona afadhali wakati wakujifungua wasaidiwe na wauguzi wa
kiume, kutokana na lugha chafu mnazowatolea", alisema Njwayo.
Mkuu
huyo wa Wilaya ambae anakaribia kutimiza miezi sita tangu ateuliwe
kushika wadhifa huo na kuhamia katika wilaya hii,aliongeza kusema licha
ya kukiuka maadili lakini pia wapo ambao siowaaminifu.
"Haiwezekani
dawa ziletwe leo, na kesho ziwezimekwisha. Gari iliyoleta ikiondoka tu,
na dawa zinakwisha" Waliosoma wapo wengi lakini hawana kazi, kama
hamtaki kuzingatia maadili basi ondokeni," alisisitiza.
Aidha
alizitaka kamati na bodi za afya kufuatilia kwa karibu matumizi ya dawa
zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuisaidia serikali kudhibiti wizi.
Mkuu huyo wa Wilaya licha ya kuweka jiwe la msingi jengo hilo ambalo
ujenzi wake umegharimu shilingi 68.06 milioni, lakini pia alizilipa
ruzuku kaya maskini 176 zilizopo katika kijiji hicho. Ikiwa ni awamu ya tatu ya utekelezaji wa mpango huo yanayofanywa na TASAF katika wilaya hii.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Miteja, Ibrahimu Msati, aliiomba serikali
kumpeleka mganga katika zahanati hiyo ambayo pia inawahudumia wananchi
wa vijiji jirani vitatu.
Post a Comment