Arsenal dhidi ya Everton
Arsenal ilijibu
kuondolewa kwake katika kombe la vilabu bingwa Ulaya pamoja na lile la
FA baada ya kuishinda Everton katika uwanja wao wa Goodison Park.
Danny
Welbeck aliiweka kifua mbele Arsenal baada ya kufunga katika dakika ya
saba ya kipindi cha kwanza baada ya kupata pasi kutoka kwa Sancheza na
kumchenga goli kabla ya kufunga.Katika dakika ya 42 Kijana Alexi Iwobi aliwafurahisha mashabiki wa Arsenal baada ya kufunga bao lake la kwanza katika kilabu hiyo.
Ni ushindi wa kwanza wa Arsenal katika mechi nne za ligi ya Uingereza.
Everton ilishambulia mara mbili pekee katika lango la Arsenal.
Post a Comment