Rais Museveni na Rais Kenyatta mwezi Oktoba mwaka 2015
Muda mfupi baada ya
Rais Yoweri Museveni kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini
Uganda, ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta akimpongeza kwa ushindi wake
ulipakiwa kwenye kurasa zake Twitter na Facebook.
“Nina furaha
sana kumpongeza Mtukufu Rais Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa tena kuwa
Rais wa Jamhuri ya Uganda. Watu wa Uganda wamenena, na wamenena kwa
uwazi. Tunaheshimu uamuzi wao wa Rais Museveni.”Rais Kenyatta alisema Kenya inathamini sana urafiki wa karibu ambao umekuwepo na kwamba anatarajia urafiki huo pamoja na ushirikiano hasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki utaendelea.
“Namtakia Rais Museveni ufanisi anapoendelea kutumikia taifa lake kwa muhula mwingine. Yeye na Uganda wanaweza kutarajia uungaji mkono wangu, na urafiki kutoka kwangu, pamoja na kutoka kwa kaka na dada zao hapa Kenya.”
Lakini hatua hiyo haikuwafurahisha baadhi ya Wakenya mtandaoni na wengi waliandika wakimshutumu.
Saa chache baadaye, kitambulisha mada#UhuruIsNotKenyakikaanza kuvuma kwenye Twitter. Kwenye Facebook, wengi waliandika kumkosoa.
Wengine walishangaa ni kwa nini Rais Kenyatta akaharakisha kumpongeza Rais Museveni ilihali “alichukua muda kumpongeza Dkt John Magufuli” alipotangazwa mshindi Tanzania”.
Kesi dhidi ya Rais Kenyatta iliondolewa lakini kesi dhidi ya Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang inaendelea.
Rais Museveni amehudhuria sherehe kadha za kitaifa na kupewa muda wa kuwahutubia wananchi.
Post a Comment