0


 mchezaji wa timu ya New generation akirusha mpira


Mchezaji wa timu ya Sido fc 
 
Timu ya Sido fc imeweza kuichapa timu ya New Generation mabao 4 kwa 3 kwa njia ya mikwaju ya penaiti baada ya kumalizika kwa 90 zikiwa hazikufungana.

Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Alizeti cup ulitimua vumbi kwenye uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Timu ya New Generation ilikuwa ya kwanza kupiga mkwaju wa penaiti iliweza kufumania vyavu mara 3 huku mlinda mlango wa Sido fc ikikamata moja na shuti linginge wakipaisha juu nao Sido fc waliweza kufumania vyavu mara 4 na kupaisha shuti moja juu.

Mchezo huu ukuwa umeudhuliwa na mashabi wengi kutoka kila kona ya mjini wa Liwale kwakuwa timu hizo ikiwa mara ya kwanza kukutana huku zikitokea katika mtaa mmoja.

Katika mashinda haya ya kanda katika kanda ya Liwale mjini zimeweza kufunzu timu 2 ambazo ni Hawili fc na Sido fc zitaungana na timu zingine mbili kutoka kila kanda ya Makata,Mihumo na Kibutuka na kufanya jumla ya timu 8.

Post a Comment

 
Top