Wahamiaji wanaendelea kufa maji wakijaribu kuingia Ulaya
Mashua mbili
zilizokua zikielekea Ugiriki zimezama karibu na Uturuki na kuwaua
wahamiaji 33. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki.
Taarifa
zinasema wahamiaji 22 walizama karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos.
Wengine 11 walizama kusini kwa Uturuki katika mkoa wa Izmir.Taarifa hizi zinajiri wakati Chancela wa Ujerumani Angela Merkel amewasili Uturuki kujadili jinsi ya kuthibiti idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya.Uturuki imewazuia maelfu ya raia wa Syria wanaokimbia mashambulizi ya jeshi la serikali katika mji wa Aleppo.
Post a Comment