0
Uganda yafunga mitandao ya kijamii
Uganda imefunga mitandao ya kijamii imefungwa kote nchini humo katika siku ya uchaguzi wa urais.
Rais Yoweri Museveni amejitetea akisema nia ya serikali yake ni kuzuia waganda kueneza uongo kuhusu uchaguzi mkuu unaoendelea .
Mitandao ya Facebook, Twitter, Whatsapp na huduma za kutuma na kupokea pesa zimefungwa.
Licha ya hatua hiyo iliyokosolewa na waganda wengi,kibwagizo cha #UgandaDecidesis kingali kinapata umaarufu mkubwa haswa kwenye mtandao wa Twitter.
Vilevile penye nia pana njia,waganda wengi akiwemo kiongozi wa upinzani na muaniaji kiti cha urais Amama Mbabazi wamepata njia mbadala ya kuwasiliana wakitumia anuani ya mtandao binafsi ya VPN - ( Virtual Private Network)
VPN ni NINI ?
 
Amama Mbabazi wamepata njia mbadala ya kuwasiliana wakitumia anuani ya mtandao binafsi ya VPN
VPN ni njia ambayo kifaa cha kielektroniki kinaweza kutumia anuani binafsi ya mtandao unaotumika katika mataifa jirani kama vile Kenya Sudan kusini na hata Marekani.
Mkuu wa idara inayothibiti sekta ya mawasiliano nchini Uganda bwana Godfrey Mutabazi, ameiambia BBC kuwa hatua ya kufunga mitandao ya kijamii imechukuliwa kufuatia ombi la baraza linalosimamia uchaguzi nchini Uganda.
Mutabazi amesema kuwa mitandao hiyo imefungwa ilikuzuia watu kuitumia kutuma hongo ili kuwashawishi wapiga kura.
Kampuni inayoongoza kwa wingi wa watumiaji ni MTN, ambayo inazaidi ya wateja milioni 10.
MTN imethibitisha kuwa imeamrishwa ifunge huduma hizo za mitandao ya kijamii.
Waganda wengi walikuwa wamekwenda kwenye mitandao ya kijamii kuelezea hasira zao baada ya vituo vya kupigia kura kuchelewesha kuanza kwa shughuli ya uchaguzi kwa zaidi ya hata saa 5.
Tume ya uchaguzi imekiri kuwa ilikabiliwa na changamoto nyingi katika usafirishaji wa makaratasi ya uchaguzi.
 
MTN imethibitisha kuwa imeamrishwa ifunge huduma za mitandao ya kijamii.
Tume hiyo imesema vituo vilivyoathirika vitaongezewa muda wa kupiga kura.
Museveni, mwenye umri wa miaka 71, anawania kuhifadhi kiti chake kwa muhula wa tano na kuendeleza utawala wake uliodumu kwa miaka 30 sasa.
Huu ndio uchaguzi wa kwanza ambao rais Museveni anakabiliwa na ushindani mkubwa zaidi kutoka kwa kiongozi wa upinzania kanali mstaafu Kizza Besigye.
Museveni amejitetea akisema nia ya serikali yake ni kuzuia waganda kueneza uongo kuhusu uchaguzi mkuu unaoendelea
Uchaguzi ulisimamishwa katika kituo kimoja katika mji mkuu wa Kampala Uganda kufuatia makabiliano baina ya polisi na vijana waliokerwa na masharti ya polisi.
Museveni anakabiliwa na wapinzani 7 katika uchaguzi huu.
Hata hivyo mpinzani wake mkuu kanali mstaafu Kizza Besigye anadai uchaguzi huu hauendeshwi katika njia ya ukweli na uhuru.
Vilevile bwana Museveni anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa mwandani wake wa karibu kwa miaka mingi bwana Amama Mbabazi.
Mbabazi aliwahi kuhudumu katika nyadhfa nyingi tu ikiwemo waziri mkuu kabla ya kufutwa kazi alipodhaniwa kupinga sera za Museveni.

Post a Comment

 
Top