Refarii mmoja
nchini Argentina amepigwa risasi na kuuawa na mchezaji aliyemuonesha
kadi nyekundu uwanjani katika mechi ya daraja la pili.
Refarii
huyo Cesar Flores alikuwa akisimamia mechi baina ya timu zinazoshiriki
ligi ya daraja la chini mjini Cordoba, takriban kilomita 700 Kaskazini
mwa Buenos Aires.Polisi wameanzisha msako mkali kumtafuta mchezaji huyo ambaye hadi sasa hajatajwa.
Refarii Flores alimuonesha kadi nyekundu mchezaji huyo na akaondoka uwanjani kama ilivyo ada.
Lakini baada ya kipindi fulani alirejea akiwa amefoka uwanjani na kumfyatulia refarii huyo risasi 3 ; Kifuani, shingoni na kichwani.
Refarii huyo mwenye umri wa miaka 48 alifariki papo hapo.
Mchezaji mwenza aliyejaribu kumshawishi asimuue refarii alipata majeraha mabaya.
Hii si mara ya kwanza kwa refarii kusini mwa Marekani kushambuliwa kutokana na uamuzi wake uwanjani.
Mwaka uliopita refarii mmoja huko Brazil alilazimika kutoa bunduki ilikumzuia mchezaji mmoja asimshambulie.
Post a Comment