Mwakilishi wa Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia Azuri Antonio Conte
anatarajiwa kukutana na yule wa klabu ya soka ya Chelsea hapo kesho
kujadili uwezekano wa muitaliano huyo kuwa kocha mpya wa The Blues msimu
ujao.
Taarifa kutoka nchini Italia zinaarifu kuwa mwakilishi wa Conte ataanza kufanya makubaliano ya awali na mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia ambaye anaripotiwa kuwasili nchini humo.
Conte ambaye aliisaidia Juventus kutwaa taji la Scudeto mara tatu mfululizo anatarajiwa kumaliza mkataba wa kuinoa timu ya taifa ya italia mwaka huu mara baada ya kumalizika kwa michuano ya mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa.
Bado tetesi zimeendelea kurindima juu ya nani atamrithi Guus Hiddink ambaye ni kocha wa muda baada ya kutimuliwa kwa Jose Mourinho huku majina mengi ya makocha yakitajwa akiwemo Massimiliano Allegri wa Juventus na Diego Simeone wa Atletico Madrid.

Post a Comment