Kituo cha mpakani chafunguliwa
Tanzania na Kenya
zimezindua huduma ya kituo cha pamoja mpakani yaani One Border Post
katika mpaka wa Holili (Tanzania)-Taveta (Kenya).
Wakizindua
huduma hiyo na majengo ya kisasa Waziri wa Tanzania anayeshughulikia
Nchi za nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na ushirikiano wa
kimataifa Balozi Agustin Mahiga na Phyillis Kandie ambaye ni Waziri wa
Kazi na Afrika Mashariki upande wa Kenya wamesema huduma hii
iliyozinduliwa ni msingi muhimu katika kuelekea kwenye Ushirikiano imara
wa Afrika Mashariki.Waziri Kandie amesema kuweka huduma za Mpaka wa Nchi mbili katika eneo moja kutakuza uchumi wa nchi zote mbili kwa haraka.
Balozi Mahiga wa Tanzania amesema hii ni moja ya hatua mojawapo za kuelekea katika matumizi ya sarafu moja.
Mradi huu ambao umechangiwa na Nchi wahisani pamoja na Kenya na Tanzania umesimamiwa na Trade Mark East Africa.
Post a Comment