0
 
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United
Kilabu ya Sunderland iliimarisha harakati zake za kuepuka kushushwa kutoka kwa ligi kuu ya Uingereza baada ya kupata ushindi dhidi ya Manchester United.
Wahbi Khazri aliiweka Sunderland kifua mbele baada ya dakika tatu za kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa adhabu uliompita kila mtu katika lango hilo.
Anthony Martial alisawazisha baada ya kuugusa mpira uliompita kipa Victor Manone ,ambaye awali alikuwa ameokoa shambulizi la Juan Marta.
Lakini Sunderland walishinda mechi hiyo baada ya kichwa cha Lamine Kone kufuatia krosi safi iliopigwa na Khazri.

Post a Comment

 
Top