Serikali
imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa iliyotolewa na Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na kusambazwa kwenye vyombo
mbalimbali vya habari kuhusu siku 100 za utawala wa Rais Magufuli kuwa
zimekandamiza Uhuru wa Habari nchini kwa kulifuta Gazeti la Mawio.Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inasisisitiza kwamba hatua
iliyochukuliwa dhidi ya gazeti la Mawio ni Sahihi na lilistahili adhabu
hiyo. Aidha, taratibu zote za kulifuta Gazeti hilo zilifuatwa ikiwa ni
pamoja na Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo kupewa nafasi ya kujitetea.Hatua
ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRCD) kutaka kujenga
taswira kwamba Gazeti la MAWIO lilionewa na kwamba halikupewa nafasi ya
kujieleza na kujitetea si sahihi na ni kuupotosha umma.Serikali
inazitaka taasisi zinazo jishughulisha na Utetezi wa Haki za Binadamu
kuacha kufanya tafsiri potofu kwa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na
Sheria nyingine za nchi. Hakuna Uhuru usio na Mipaka na Staha.Serikali
inautaarifu Umma kuwa hatua ya kutunga Sheria ya Huduma za Habari
(Media Service Bill) na Haki ya kupata tarifa inaendelea vizuri na
Wizara zinaendelea kupokea maoni ya kuboresha Miswaada hiyo.Muswaada
wa Haki ya Kupata Taarifa unasimaiwa na Wizara ya Katiba na Sheria,
Muswaada huo unawahusu watu wote. Muswaada wa Huduma za Habari ni
mahsusi kwa Wadau wote wa tasnia ya Habari.
Serikali
inatoa wito kwa wadau wote wa sekta ya habari kuchangia kuboresha
miswaada hiyo. Aidha, inawataka Wanahabari wawe mstari wa mbele katika
kuchangia uboreshaji wa Muswaada wa Huduma za Habari badala ya kuwaachia
wanataaluma nyingine kutoa maoni na maelekezo katika muswaada huo.
Serikali
inawakumbusha wananchi kwamba Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976
itaendelea kutumika mpaka pale Sheria mpya itakapopitishwa na Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika
hatua nyingine Serikali inapenda kuwataarifu wananchi kuwa suala la
urushaji wa matangazo ya “live” kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania
(TBC) lilisha tolewa ufafanuzi na Viongozi Wakuu wa Serikali. Hivyo
mjadala huo ulihitimishwa.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
13/FEBRUARI/2016.
13/FEBRUARI/2016.
Post a Comment